Unaambiwa Asilimia 52 ya Wahitimu Wanafanya Kazi Ambazo Hawajasomea – Utafiti

2 years ago115 Views

 Asilimia 52 ya wahitimu wanafanya kazi ambazo hawajasomea - Utafiti

Kulingana na ripoti iliyotolewa na kampuni ya utafiti wa data ‘Burning Glass Institute and Strada Education’ imeeleza kuwa asilimia 52 ya wanafunzi waliohitimu Degree nchini Marekani wanafanya kazi ambazo hawajasomea (hazihitaji elimu ya chuo kikuu).

Ambapo kufuatiwa na ripoti hiyo imebaini kuwa ndani ya mwaka mmoja hadi mitano ya kuhitimu na kukosa ajira, wahitimu hao huchukua uamuzi wa kufanya kazi ambazo hawajasomea zikiwemo, uhudumu wa chakula, usaidizi katika ofisi, wafanyausafi, ujenzi, pamoja na kujishugulisha na biashara.

Ripoti hiyo, iliyotolewa siku ya juzi Alhamis imezua gumzo kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuona idadi kubwa ya wahitimu wakifanya kazi ambazo hawajasomea.

Hata hivyo waandishi wa ripoti hiyo walimalizia kwa kuwashauri wanafunzi kuelewa mapema hatua za kuchukua ili kupunguza kukosa ajira pindi watakapo hitimu. .

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.