UKAWA WATOFAUTIANA,WASHINDWA KUELEWANA..SOMA HAPA

Admin Updates11 years ago4 Views

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umeendelea kushikilia hatima ya
kupatikana kwa Katiba Mpya yenye maridhiano ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, inayopaswa kupendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba kwa
wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.


Hata hivyo, licha
ya UKAWA kuhodhi upatikanaji wa Katiba Mpya yenye maridhiano, taarifa
zinabainisha kwamba uamuzi wa jumla wa wajumbe wake wa Bunge la Katiba
kutoshiriki mkutano ujao wa Bunge hilo umeanza kuingia dosari, mgongano
wa kimtazamo ukianza kuibuka.


Kwa mujibu wa taarifa za uhakika
ambazo gazeti hili limezipata kutoka kwa vyanzo kadhaa vya habari, UKAWA
imegawanyika kimtazamo katika mapande mawili kwa sasa.


Upande
mmoja ni ule wenye msimamo wa kutokurejea bungeni hadi pale Rasimu ya
II ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyowasilishwa katika Bunge
Maalumu la Katiba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph
Warioba itakaporidhiwa kujadiliwa bila kutiwa viraka vikubwa.


Kwa
mfano, kati ya viraka ambavyo kundi hilo la UKAWA halivitaki ni kile
kinachopachikwa kuziba muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye
Serikali tatu, ambalo ndilo pendekezo la Tume ya Warioba.


Kundi
hili linapingana na mapendekezo ya muundo wa Serikali mbili ambao
unapigiwa chapuo na wajumbe wa Bunge Maalumu wengi kutoka Chama cha
Mapinduzi (CCM).


Kundi hili linawajumuisha baadhi ya viongozi
wakuu wa vyama vya siasa walioko ndani ya Bunge la Katiba na wale
walioko nje ya Bunge hilo.


Hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Katibu Mkuu
wake, Dk. Wilbroad Slaa.


Wengine katika kundi hili ni James
Mbatia ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la Katiba na Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, Profesa Ibrahim Lipumba – Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi
(CUF) na mjumbe wa Bunge la Katiba.


Lakini katika kundi la pili,
wamejitokeza baadhi ya viongozi waandamizi wa upinzani ambao wanaamini
si hatua muafaka kususia mkutano wa Bunge la Katiba.


Katika kundi
hili, viongozi hao wanaungana na ushauri uliowahi kutolewa na Rais
Jakaya Kikwete kwamba, mahali muafaka katika kusaka suluhu ya mtanziko
uliojitokeza kati ya wajumbe wa Bunge la Katiba ni katika Bunge hilo
hilo, kupitia Kamati yake ya Maridhiano.


Katika hali hiyo, vyanzo
vya habari vya gazeti hili vimedokeza kwamba kundi la kwanza linatumia
zaidi mikutano ya hadhara kuhamasisha wananchi lakini kundi la pili,
haliamini katika mbinu hiyo.


Kwamba mbinu ya mikutano ya hadhara
haina tija inayojitosheleza dhidi ya kutumia kamati za Bunge, ikiwamo
Kamati ya Maridhiano, kutafuta suluhu.


Lakini akizungumzia hatua
za kutafuta suluhu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa, Jumanne wiki hii,
alimwambia mwandishi wetu kwamba; “maoni ya wananchi hayawezi kutafutiwa
suluhu hata kidogo, bali yanapaswa kuheshimiwa tu.”


Wakati Dk.
Slaa na wenzake katika kundi la kwanza la UKAWA wakiamini hivyo, taarifa
za uhakika zinabainisha ya kuwa, utayari wa baadhi ya wajumbe wa UKAWA
kurejea kwenye Bunge la Katiba umekwishakujipambanua.


“Baadhi
yetu, baada ya kufanya mikutano kadhaa ya hadhara, licha ya mikutano
hiyo kufanikiwa lakini tathmini yetu inatuelekeza kwamba ni muhimu
kurejea bungeni, kusimamia hoja ambazo tumezifafanua kwa wananchi
mikutanoni, ikishindikana tutaendeleza harakati zetu wakati wa kampeni
kuelekea upigaji kura ya maoni.


“Bunge la Katiba tumebaini ni sehemu muafaka kwetu kuendelea kupaza sauti juu ya kile tulichokisema kwenye mikutano ya hadhara.

“Na
katika hali ya kutetea hayo, bila shaka wenzetu wanaweza kutuelewa
wakakubaliana nasi au sisi na wao tukatafuta muafaka wa ‘katikati’ wenye
kubeba maslahi ya nchi,”
alisema mmoja wa viongozi waandamizi wa
upinzani kutoka Zanzibar, ambaye ni mjumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba-UKAWA.


Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta pamoja
na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan, hawakuweza
kupatikana kufafanua kuhusu juhudi zao kuwashawishi UKAWA kurejea
bungeni.


Hata hivyo, Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Hamad
Khamis Yahya, alimweleza mwandishi wetu kwamba suala la kuwashawishi
UKAWA kurejea bungeni ni la kisiasa zaidi na si la kiutendaji na kwa
hiyo, kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na ofisi ya Mwenyekiti wa Bunge hilo.


Alisema
wao, wakiwa ni watendaji wakuu wa Bunge la Katiba wanachofanya kwa sasa
ni kuweka mpangilio wa shughuli za Bunge ili zikamilike ndani ya siku
60 zilizoongezwa na Rais Jakaya Kikwete, kwa ajili ya kukamilisha kazi
ya kuandika Katiba Mpya itakayopigiwa kura ya maoni na wananchi.


Aprili
16, mwaka huu, UKAWA wenye wajumbe takriban 200 wakiongozwa na Profesa
Ibrahim Lipumba walisusia vikao vya Bunge la Katiba kwa madai kwamba,
kuna mpango wa kuvuruga mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya
Katiba.


Katika ushawishi wake kwa wenzake, Lipumba akiwa ndani ya
ukumbi wa Bunge siku hiyo saa 10:31 jioni, alisema: “UKAWA hatuwezi
kuendelea kushiriki dhuluma dhidi ya wananchi kwa kupitisha Katiba
ambayo ni kinyume cha matakwa yao.”

 


Makala hii imenukuliwa   kutoka kwenye gazeti la RAIA MWEMA “Mgongano UKAWA


0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.