Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Flugence Ngonyani, alisema Mwinjilisti Milenyi aliuawa Septemba 8, mwaka huu saa 1:14 jioni katika Kijiji cha Mahongo Mterini.
Kamanda Ngonyani alisema mwinjilisti huyo, aliuawa kwa kupigwa kwa mishale miwili sehemu ya shavu la kushoto na mwingine mgongoni na watu ambao hadi sasa hawajafahamika wakati akirudi nyumbani kutoka shambani.
“Mwinjilisti huyu, alikuwa anatoka shambani kwake kurudi nyumbani, alikutana na watu ambao hawajafahamika, walichoma mishale miwili kwenye shavu lake la kushoto na mgongoni na kumsababishia kifo chake papo hapo,” alisema Kamanda Ngonyani.
Alisema chanzo cha mauaji hayo, hakijafahamika na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma kwa uchunguzi zaidi wa daktari.
Alisema Jeshi la Polisi linandesha msako mkali ili kuwabaini waliohusika na mauaji hayo.
Wakati huo huo, Kamanda Ngonyani alisema Sweetberth Magila (48), mwalimu wa Shule ya Sekondari Minja, ameuawa kwa kuchomwa kisu na mkewe kutokana na wivu wa kimapenzi.
Alisema tukio hilo lilitokea Septemba 9, mwaka huu saa 2:20 usiku katika Kijiji cha Masumeni wilayani Mwanga.
Kamanda Ngonyani alisema mwanamke huyo, Tumaini Magila (27), mwalimu wa Shule ya Sekondari Minja, alimchoma mumewe kisu kwenye paji la kushoto.
Alisema baada ya kumchoma kisu, alivuja damu nyingi na kufariki dunia.
Alisema kabla ya mauaji hayo, inadaiwa wanandoa hao walikuwa wakiishi pamoja, lakini wakiwa na ugomvi wa mara kwa mara kutokana na wivu wa kimapenzi huku mkewe akimtuhumu mumewe kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine.
“Kabla ya mauaji haya, walitoka pamoja kwenda kunywa pombe na baadae walirudi nyumbani, ambako baada ya muda walianza kugombana na kuanza kupigana… Wakati wakiendelea na ugomvi, mke alichukua kisu na kumchoma mume wake,” alisema Kamanda Ngonyani.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa Hosptali ya KCMC kwa uchunguzi zaidi na wanamshikilia Tumaini kwa upelelezi zaidi.
NA UPENDO MOSHA, KILIMANJARO>>>Mtanzania
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






