RC Rosemary Senyamule asisitiza uadilifu na uwajibikaji katika utekelezaji wa Miradi Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema ushirikiano, uwajibikaji na uadilifu ni msingi muhimu wa kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali inaleta matokeo yaliyokusudiwa na kuwanufaisha wananchi.
Akifungua warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa wadau wa usimamizi wa miradi ya maendeleo, Julai 21, 2026, Mhe. Senyamule alisema warsha hiyo inalenga kuimarisha uwajibikaji, kuongeza ushirikiano kati ya TAKUKURU na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya rushwa, pamoja na kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika kwa ufanisi, uwazi na kwa manufaa ya wananchi.
Alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza fedha nyingi katika sekta mbalimbali za maendeleo ili kuboresha huduma za kijamii na kukuza uchumi.
“Sehemu kubwa ya bajeti ya Serikali inaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo kwa kuwa ndiyo chachu ya ukuaji wa uchumi na uboreshaji wa huduma katika sekta za afya, elimu, maji, miundombinu na nyinginezo. Hivyo ni wajibu wa kila mdau kuhakikisha fedha za Umma zinasimamiwa kwa uwazi, ufanisi na uadilifu ili miradi ikamilike kwa wakati na kuleta manufaa yaliyokusudiwa,” alisema Mhe. Senyamule.
Alisisitiza kuwa usimamizi madhubuti wa miradi unahitaji ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za Serikali, TAKUKURU, viongozi na wananchi ili kuziba mianya ya ubadhirifu na vitendo vya rushwa vinavyoweza kuathiri utekelezaji wa miradi.
Aidha, aliwataka washiriki wa warsha kutumia maarifa watakayopata kuimarisha ufuatiliaji wa miradi katika maeneo yao, kubaini changamoto mapema na kuchukua hatua stahiki ili kuzuia kujirudia kwa mapungufu yaliyowahi kujitokeza.
Alieleza kuwa utekelezaji wa miradi kwa kuzingatia viwango vya ubora, thamani halisi ya fedha na muda uliopangwa utaongeza imani ya wananchi kwa Serikali na kuharakisha maendeleo ya Mkoa wa Dodoma na Taifa kwa ujumla.
Mhe. Senyamule pia aliwahimiza wadau wote kutekeleza majukumu yao kwa bidii, weledi na uadilifu bila kusubiri kusukumwa, akisisitiza kuwa kila mmoja ana wajibu wa kulinda rasilimali za umma kwa manufaa ya wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Christopher Mayans, alisema Serikali imeendelea kutenga fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali, hivyo mafanikio ya uwekezaji huo yanategemea usimamizi madhubuti kuanzia hatua ya upangaji, uidhinishaji, utekelezaji, usimamizi wa mikataba hadi kukamilika kwa miradi.

Aliongeza kuwa TAKUKURU inaendelea kutekeleza wajibu wake wa kisheria wa kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma katika miradi ya maendeleo kwa lengo la kubaini mapema changamoto na kasoro zinazoweza kuathiri uwazi, ufanisi na thamani ya fedha za umma.

SOMA MAKALA HIZI NYINGINE MUHIMU HAPA
RC Senyamule aelekeza Vikundi zaidi ya 300 Jijini Dodoma Vipewe mikopo Tsh Bilioni 3.6
RC Nurdin Babu awataka wageni wanaowasili Kilimanjaro kulinda amani.
RC Batilda Buriani:Tanga tumepata Zaidi ya Bilioni 429 kutekeleza haya Makubwa
DC Grace Kingalame ataka watoto wenye sifa kuanza shule mara moja Nyang’wale,awaonya wazazi wanaowatumikisha na kuwazuia
MAMLAKA YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI (DCEA) YATEKETEZA SHAMBA LA BANGI ZAIDI YA HEKARI 100..SOMA ZAIDI HAPA
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






