Tume ya Uchaguzi yabadili majina ya Majimbo matatu, yatangaza zoezi la utoaji fomu (+video)

Special Correspondent4 years ago5 Views


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, ametangaza ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu kwa ajili ya Urais kuwa ni August 5 hadi 25, 2020.

Aidha, fomu za nafasi ya Ubunge na Udiwani zitatolewa kuanzia August 12 hadi 25, 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma, Jaji Kaijage, amesema fomu kwa ajili ya Urais zitatolewa katika Ofisi ya tume hiyo zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma na nafasi ya ubunge na udiwani zitatolewa katika Ofisi za uchaguzi zilizopo katika halmashauri na kata husika.

Jaji Kaijage, ametaja kubadilishwa kwa majina ya majimbo ambapo Jimbo la Chilonwa litaitwa Chamwino, Mtera linaitwa Mvumi na Kijito Upele lililopo Mjini Magharibi linaitwa Pangawe.

Ametaja idadi ya majimbo kuwa ni 264 Kama ilivyokuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo 214 yapo Tanzania Bara na 50 yapo Zanzibar na kata 3,956.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.