Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed A. Ahmed leo tarehe 6 Agosti,2024 ameshuhudia utiaji saini wa mikataba 50 yenye thamani ya shilingi bilioni 14 baina ya TARURA na Wakandarasi kwaajili ya matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa mkoa wa Ruvuma kwa mwaka 2024/2025
Menaja wa TARUR AMkao wa Ruvuma akimkabidhi mmoja wa wakandarasi Mkataba wake mjini Songea.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela ameshuhudia utiaji saini wa mikataba 24 baina ya TARURA na Wakandarasi yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.6.
Katika hafla hiyo Mhe. Shigela amewataka wakandarasi hao kukamilisha miradi yao mapema na kwa viwango vyenye ubora ili kuendelea kutengeneza uaminifu kwa serikali na hivyo kupewa kazi nyingine.
Naye,Meneja wa TARURA Mkoa wa Geita Mhandisi David Msechu amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya shilingi bilioni 20.3 zimeidhinishwa na serikali kwa ajili ya ujenzi,ukarabati na matengenezo ya barabara mkoani humo.