Kama jinsi ambavyo watanzania tunatumia vibaya mitandao kwa kuumizana
kwa njia ya matusi na kuchafuana, wana siasa wetu waliopitisha hii
Sheria ya cybercrime pia wameitumia vibaya hii Sheria na kuitumia kama
silaha ya kumfunga mdomo mtanzania.
Kusema ukweli mimi kama Wema Sepetu nimechoka kutukanwa, mpaka mama
yangu mzazi anadhalilishwa humu Kwenye mitandao. Kuna kipindi nilifikia
hatua ya kuwaza bora nife tu ili kuepukana na matusi na kuandikwa na
magazeti kwa habari za uongo.
Lakini as much as ningependa Kuwe kuna Sheria kama hii ya kunisaidia
mimi Wema niepukane na matusi Naona ni bora niendelee kutukanwa mpaka
Siku nitakayokufa kuliko kuona fans wangu mimi, fans wa Wolper, fans wa
Jokate, fans wa Ali Kiba, fans wa Diamond Platinumz na Wengine wengi
wakinyang’anywa haki yao ya msingi kabisa ambayo ni haki ya kuweza
kufungua mdomo na kuongea hata yale ambayo sisi mastar na wanasiasi
hatukubaliano…..Je mimi kama Wema nitasemaje nawadhamini fans wangu
ambao wao ndo wamenipa umaarufu huu na kunifikisha hapa nilipo kama hapo
hapo nitawanyanyasa kwa kuwapokonya haki yao ya freedom of speech.
Mimi Wema sijakamilika , wote mnajua ninamapungufu yangu , je mimi Wema
nitawezaje kujua makosa yangu ili niweze kubadilika na kufanyA vizuri
kama sitokubali kusikiliza maoni ya watu wote yawe mabaya au
mazuri?Nafikir wore mnajua hakuna page ya Mtanzania hapa instagram yenye
matusi na malumbano kama page yangu mimi ….
Nimeshauriwa sana Kuwa nianze kublock wote wanaoniwekea comment za
matusi na kufuta comments zao kama wanavyofanya mastaa wengine lakini
nimegoma. Je mnadhani mimi nafurahia hizo comment za matusi? Tena Kwenye
page yangu mwenyewe? Hapana zinaniumiza ila pia nakumbuka Kuwa mimi ni
kioo cha Jamii nakumbuka Kuwa kabla ya Wema sepetu first comes nchi
yangu …..
Niko tayari nitukanwe lakini haki za fans wangu, haters wangu na
watanzania wote kwa ujumla ziwe po pale pale. Watanzania naomba tuungane
katika kumsupport my dada Kwenye hili @iworeadress @iworeadress. Mimi
nimemwelewa sana anachokisema. Tunaelekea pabaya Sasa….Tupiganie haki
zetu za uhuru wa kuongea. Tusipojipigania hakuna wa kutupigania. Naamini
Chama changu nachokipenda cha CCM kitatusikukiza wananchi wake na
kufanyia hilo kazi.Tafadhali follow hii page ili tuweze kuchangia na
kabadilishana mawazo . @ccmchangeorquit
By Wema Sepetu on Instagram