SOMA HII TAARIFA MUHIMU TOKA OFISI YA KATIBU MKUU WA CCM MHE.DANIEL CHONGOLO

Admin Updates3 years ago4 Views

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo atakuwa na Ziara ya Kikazi Mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Katavi na Tabora akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Ziara hiyo itaanza Tarehe 13 – 24 Novemba, 2021 Mkoani Kagera katika Wilaya zote za Mkoa huo, na kuendelea katika Mikoa ya Geita, Kigoma, Katavi, na kuhitimisha mkoa wa Tabora.
Malengo ya ziara hiyo ni kuimarisha Uhai wa Chama katika ngazi za Mashina pamoja na Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, ikiwa ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa cha  tarehe 29 Juni, 2021.
Wajumbe wa Sekretarieti watakaojumuika katika Ziara na Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM – Bara Ndg. Christina Mndeme, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg. Kennan Kihongosi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Dkt. Philis Nyimbi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Ndg. Gilbert Kalima.

 

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.