Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo atakuwa na Ziara ya Kikazi Mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Katavi na Tabora akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Ziara hiyo itaanza Tarehe 13 – 24 Novemba, 2021 Mkoani Kagera katika Wilaya zote za Mkoa huo, na kuendelea katika Mikoa ya Geita, Kigoma, Katavi, na kuhitimisha mkoa wa Tabora.
Malengo ya ziara hiyo ni kuimarisha Uhai wa Chama katika ngazi za Mashina pamoja na Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, ikiwa ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa cha tarehe 29 Juni, 2021.
Wajumbe wa Sekretarieti watakaojumuika katika Ziara na Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM – Bara Ndg. Christina Mndeme, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg. Kennan Kihongosi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Dkt. Philis Nyimbi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Ndg. Gilbert Kalima.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







