SIMANZI: Hivi ndivyo Ajali ya Prado na Lori ilivyoua hawa ndugu wanne Mbwewe

Admin Updates1 year ago5 Views

Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limethibitisha vifo vya Watu wanne (Ndugu wa Familia moja) ambao wamefariki baada ya gari aina ya Toyota Prado walilokuwa wamepanda wakitokea Dar es salaam kwenda Same, Kilimanjaro kugongana uso kwa uso na Scania lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es salaam.

RPC wa Pwani Piusi Lutumo amesema ajali imetokea saa nane usiku wa kuamkia leo eneo la Mapatano Kata ya Mbwewe Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani na waliofariki ni Dereva wa Prado Nechi Msuya (45-50), Mkurugenzi wa Benki ya ABSA na Mkazi wa Dar es salaam pamoja na Watu watatu waliokuwa kwenye gari hilo ambao ni Dayana Mageta(40-45), Norah Msuya (40-45) na Ndugu mwingine wa kike.
Kamanda Lutumo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Prado ambaye alihama upande wake na kugongana uso kwa uso na Scania “Mili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Zahanati ya Lugoba kwa ajili ya uchunguzi na kutambuliwa na Ndugu”
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.