JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –
Nimemsimamisha kazi kwa Muda Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Bandari Ndgu.Madeni Kipande leo hii trh 16 Februari 2015 ili kupisha
uchunguzi unaohusu tuhuma mbalimbali zinazomkabili.
Tuhuma hizo ni Pamoja na manung’uniko kuhusiana na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi .Hali hii inatokana na kutotabirika kwa taratibu na kukosekana kwa uwazi , pamoja na taratibu hizo kuingiliwa na mamlaka.
Aidha tuhuma nyingine ni mahusiano yasiyoridhisha kati ya Uongozi wa
Mamlaka ya Bandari na wadau wake muhimu na Mahusiano mabaya sehemu ya
kazi.
Kufuatia hali hii,nimeteua Tume ya kuchunguza suala hili
na nimeipa muda wa wiki mbili Kukamilisha kazi hii na kunipatia
taarifa. Majina ya Tume hiyo ni Kama ifuatayo :-
1.Jaji Mstaafu Agusta Buheshi-Mwenyekiti.
2.Ndgu.Ramadhan Mlingwa-Mjumbe
3.Eng.Samson Luhigo-Mjumbe
4.Ndgu.Happiness Senkoro-Mjumbe
5.Ndgu.Flavian Kinundo -Mjumbe
6.Ndgu.Deogratius Kasinda-
Katibu
Wakati Ndgu.Kipande akiwa amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, kwa
mujibu wa Mamlaka niliyopewa na sheria ya Bandari Namba 17 ya Mwaka
2004 Kifungu Cha 34 Kifungu kidogo cha 2 ninamteua Meneja wa Bandari
Dar Bwana Awadh Massawe kukaimu nafasi hiyo kuanzia leo trh 16 Februari
2015.