RC Rosemary Senyamue: Matokeo ya ziara ya Kidiplomasia ndani ya Jiji la Dodoma yameanza kuonekana

Masama BlogMATUKIOKIMATAIFASIASAKITAIFAYesterday16 Views

Matokeo ya ziara ya Kidiplomasia ndani ya Jiji la Dodoma iliyofanyika Mei 27, 2025 yameanza kuonekana kufuatia Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Saudi Al Hilal Shidhani kukabidhiwa hati ya ujenzi wa kituo cha utamaduni cha Ubalozi huo kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la viwanja vya Mabalozi lililopo Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.

Hati hiyo iliyotolewa na Mkoa wa Dodoma, ilikabidhiwa kwa Balozi huyo na Waziri mwenye dhamana ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Thabit Mahmoud Kombo katika hafla iliyofanyika June 05, 2025 kwenye Ofisi ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Mhe. Kombo amesema kituo hicho hakitakua tu mahali pa kuhifadhia na kuendelezea utamaduni, bali pia kitakua kivutio kwa Wanataaluma, Watafiti na Wanafunzi kutoka Mataifa mbalimbali hivyo, kusaidia kuongeza mapato ya Utalii na kuchangia kukuza uchumi wa Dodoma na Taifa kwa ujumla.

Balozi huyo wa Oman Nchini amemshukuru Mhe.Rais kwa kutoa kiwanja hicho,na kuongeza kuwa Serikali yake imeshajipanga kuanza mchakato wa ujenzi wa kituo hicho kitakachokuwa cha kisasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ambaye hivi karibuni aliandaa ziara ya Mabalozi (Capital City Diplomatic Tour) kutembelea miradi mbalimbali ya kimkakati iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali Jijini hapa, ameeleza jinsi Mkoa ulivyojipanga kujenga mji janja ( Hombolo Thermatic City) kutenga eneo kwa ajili ya tamaduni za makabila yote Nchini na nchi nyingine Duniani kwa kaulimbiu ya ‘Take Dodoma to The World and Bring The World to Dodoma’na kuifanya Dodoma kuwa kati ya Majiji ya kisasa na ya kuvutia Duniani.Aidha amewakaribisha wadau wengine kuja kuwekeza Dodoma .

Leave a reply

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...