Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Tixon Nzunda (Pichani)na dereva wake wamefariki kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la KIA wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kwamba imetokea majira ya saa nane mchana leo Juni 18, 2024.
“Ni kweli wakati anatoka KIA amepata ajali mbaya sana, ndio na mimi nakwenda eneo la ajali,”amesema RC Babu
Muda mfupi kabla ya ajali hiyo, alikuwa na kikao na wadau wa maendeleo kutoka nchini Namibia kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo
Katika ajali hiyo inadaiwa kuwa, dereva wake naye amefariki dunia.