Rais Samia Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Utendanji Kazi wa PAUL Makonda

2 years ago126 Views

 Rais Samia Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Utendanji Kazi wa PAUL Makonda

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Paul Makonda amefanya kazi nzuri CCM akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa ya kukichemsha Chama na kufanya hata waliokuwa Wavivu kuamka ambapo amesema amempeleka Arusha kuwa Mkuu wa Mkoa na ana matumaini nae makubwa kuwa atafanya kazi nzuri kama aliyoifanya akiwa RC Dar es salaam.

Akiongea leo April 04,2024 Ikulu Dar es salaam wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali, Rais Samia amesema “Paul Makonda umefanya kazi nzuri CCM, umekichemsha Chama, ilikuwa Chama kidogo kina kila mmoja Mvivu kutoka hataki sinziasinzia lakini umeingia njiani umekichemsha Chama tumeamka vizuri sana lakini najua kwamba ulikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kwenyewe ulifanya mazuri makubwa”

“Tumekupeleka Arusha, unajua nini kipo Arusha na unajua matumaini yangu kwako Arusha, nenda kafanye kazi Arusha Mimi nina imani kubwa nawe na najua utafanya kile ambacho Mimi natamani ukafanye”

“Kubwa kwenye Arusha Utalii umekua vizuri sana, Wageni ni wengi malazi hakuna kwahiyo nenda kasimamie ukisaidiana na Uwekezaji kuhakikisha tunapata malazi mengi sana kwa ajili ya Wageni wetu, Arusha ni Mji Mkubwa sana ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini Mataasisi mengi ya Kimataifa yapo Arusha kwahiyo nenda kasimamie vizuri Mkoa uwe na jina zuri

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.