PICHA: ANGALIA FUMANIZI LA AIBU MKE NA MUME WA MTU USIKU WA MANANE GESTI JIJINI DAR HILI HAPA LIVE!

Admin Updates10 years ago5 Views

Mwanamke aliyefumaniwa gesti akijivinjari na mume wa mtu.
MAPEMA ASUBUHI TULIITOA STORI HII BILA PICHAZ! ENJOY SASA LIVE!Issa Mnally na Richard Bukos
AMA
KWELI duniani kuna mambo! Wakati wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam
wakiwa katika harakati za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, dada mmoja
ambaye ni mke wa mtu yeye alijikuta akiiserebukia kwa fumanizi gesti,
tena akiwa na mume wa mtu!

Tukio hilo lilijiri Alhamisi Kuu
maeneo Buza jijini Dar, mishale ya saa 7:00 usiku huku jamii ikiwa
katika harakati za kununua hiki na kile kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka
iliyoadhimishwa duniani kote jana huku leo ikiwa ni Jumatatu ya Pasaka.

…akivaa
nguo zake ili wapelekwe kituo cha polisi. Katika fumanizi hilo,
timbwili la aina yake liliibuka baada ya mwanamke huyo mwenye mwili
mkubwa, kuponyoka mikononi mwa mke aliyemnasa na kutoka nduki nje akiwa
mtupu bila kujali hali hiyo.

…akichukua vitu vyake na kupakia kwenye mkoba tayari kwa kupelekwa kituo cha polisi. MADAI YA AWALI
Awali, ilidaiwa kuwa mume huyo wa mtu aliyefahamika kwa jina la baba
Somoe, mkazi wa Kongowe (nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam)
alimchepuka mke wake (mama Somoe) na kuanzisha uhusiano na mwanamke
huyo.

…akijitetea kwa mgoni wake wakati wakipelekwa kituo cha polisi. MKE ATILIA SHAKA, AFUATILIA
Chanzo kikazidi kudai kwamba mkewe huyo alianza kutilia shaka mwenendo
wa mumewe kutokana na kubadili tabia, hasa za kuwa beneti na simu hivyo
alianza kumfuatilia kwa karibu.
“Katika kumfuatilia, siku moja
akabaini meseji. Akamuuliza mumewe kuhusu meseji hiyo naye akawayawaya
bila kuwa na majibu sahihi,” kilisema chanzo hicho.

MKE AWEKA MASHARTI MAGUMU
Habari
zaidi zilisema kuwa kutokana na ukweli kwamba, ndani ya nyumba yao,
mama Somoe ndiyo kajaliwa uwezo wa kumiliki fedha, alimpa masharti
mumewe kwamba achague mawili, watengane na aondoke na begi lake la nguo
au atoe ushirikiano, ‘mwizi’ huyo anaswe.
“Mume akasema cha kufia! Akakubali kutoa ushirikiano ili mchepuko wake afumaniwe,” kilidai chanzo chetu.

OFM WALIFIKAJE ENEO LA TUKIO?
Ni
kawaida kwa makamanda wa Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’
kinachomilikiwa na Global Publishers kuzunguka katika viunga vya Jiji la
Dar ili kusaka matukio, ndipo katika harakati hizo, wakajikuta
wameibukia mtaa wenye sekeseke hilo la aina yake.
OFM: “Kuna nini hapa?”
Shuhuda: “Kuna fumanizi. Kuna mke wa mtu amefumaniwa na mume wa mtu gesti, inasemekana ni mtego wa mke.

KUTOKA NDANI
Kelele
za ‘huyo…huyo! Jamani niacheni…hamna… umezoea leo nimekunasa, loo! Hata
aibu huna…kwani nimekufanya nini?’ zilisikika kutoka ndani.
OFM
walitinga hadi ndani ya gesti hiyo na kukuta timbwili la aina yake
ambapo mshikemshike nguo kuchanika ndiyo ilikuwa habari yenyewe.

Baada ya kubaini anapigwa picha na OFM, mwanamke huyo alitoka baruti
akikimbizwa kwa nyuma na mwanamke aliyedai amemfumania sanjari na polisi
huku picha zikiendelea kupigwa.

POLISI WAMDAKA
Nje, polisi walifanikiwa kumdaka na kumpiga pingu yeye na mwanaume aliyekuwa naye, yaani baba Somoe

MKE AZUNGUMZA NA OFM
Akizungumza na OFM baada ya utulivu kurejea huku watuhumiwa wakiwa anda aresti (chini ya ulinzi), mama Somoe alisema:
“Nimeamua kufanya hivi baada ya kuzifuma meseji nyingi za kimapenzi
katika simu ya mume wangu. Nilipombana alikiri kuwa na mchepuko nje ya
ndoa lakini aliniomba msamaha.
“Hata hivyo, pamoja na kuniomba
msamaha bado mwenendo wake haukuwa mzuri, alikuwa bize sana na simu
yake. Sasa jana (Jumatano iliyopita) alipokwenda kuoga ikaingia meseji
kwenye simu yake, akiambiwa tayari ameshawekewa chumba kwenye gesti
hii.

“Meseji hiyo ilisema hivi; kaka ulisema tukuwekee chumba
chako kile cha mauaji lakini bahati mbaya kina mgeni tangu jana,
tumekuwekea chumba namba A3. Mimi mhudumu hapa gesti…” (jina la gesti
tunalihifadhi).
Mwanamke huyo alidai kuwa akiwa na kaka yake, baada
ya kuwapata askari, walikwenda kugonga kwenye chumba hicho, walipofungua
yeye aliangua kilio baada ya kumkuta mumewe akiwa na mchepuko huo
kitandani.

KUHUSU MTEGO
Mama Somoe alisema hajui lolote
kuhusu yeye kumuwekea mtego mwanamke huyo bali anachojua ni SMS za mtu
wa gesti ndiyo ziliibua mambo.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.