PENNY NA WEMA SEPETU SASA WAFANYA PROJECT MOJA…NI HII HAPA

Admin Updates10 years ago5 Views



Imelda Mtema
STAA wa
filamu Bongo, Wema  Sepetu na Mtangazaji Penniel Mwingila ‘Penny’ ambao
wote kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya kuona habari za
mwenza wao huyo wa zamani akiwa na mpenziwe mpya, Zali zinapamba moto
kila siku, wameibuka na kudai hawababaishwi nazo, kwani hivi sasa
wameamua kuingia kazini kwa kufanya bonge la project.

Mtangazaji Penniel Mwingila ‘Penny’.


Akizungumza kwa niaba ya mwenzake, Penny alisema kelele za kila siku
wamezichoka na baada ya kukaa pamoja, wameona hiki ni kipindi cha kupiga
kazi badala ya kupoteza muda.

 
Staa wa filamu Bongo, Wema  Sepetu.


“Tumeamua kuandaa filamu yetu ya pamoja ambayo ninaamini itakuwa ni kali
na ya aina yake. Tumepoteza muda mwingi na hivi sasa tunahitaji kufanya
kazi, tunachowaomba mashabiki wakae tayari kutupokea na hatutaki tena
kushabikia mambo ya Zali na Diamond kwa sababu hayatuhusu,” alisema.


Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.