Utakuwa na Kumbu kumbu kwamba Baada ya Msanii Kutoka Arusha Dogo Janja Kutoka Nje ya Mikono ya Jambo Squad alichukuliwa na Madee wa Tip Top Connection lakini baada ya Janja Kujulikana Tanzania Nzima Kupitia Madee alimkimbia Madee na kuwa chini ya Ostaz Juma Namusoma kupitia Mtanashati Entertainment ila baadae tena Msanii huyo alirudi kwa Madee alipo Mpaka Sasa.
DOGO JANJA
Dogo Janja kwa Sasa anatamba na Wimbo wake Mpya MY LIFE ambao umempa Heshima Kubwa sana Baada ya Kukaa Kimya Kipindi Kirefu sasa na kwa Siku Chache toka Utoke Wimbo huo sasa unamuwakilisha Janja na Timu yake ya Tip Top ikiongozwa na Madee kwenye Chart Mbali mbali za Radio na Tv Nchini Tanzania.
OSTAZ JUMA
Nilianza Kumuuliza Ostaz Juma Namusoma kama anampigiaga Janjaro hata Kumsalimia Jamaa akajibu kwamba Dogo Janja Ndiye anapaswa Kumpigia yeye na Kumsalimia kwani alishawahi kuwa Boss wake japo amefuta taarifa za kwamba hawawasiliani na akasema ni juzi tu Ameongea na Dogo Janja.
Amezungumzia Pia Suala la Mahusiano kwamba Ameoa na ana Mtoto Mmoja sasa
OSTAZ JUMA NAMUSOMA AKIWA NA MKEWE
Swali la Je Anauzungumziaje Wimbo wa Dogo Janja Limeleta Majibu haya toka kwa Ostaz Juma Namusoma:-
Kwakweli Dogo Janja ni Mwanamuziki Mzuri sana hata Madee Hamfikii yaani Dogo Janja anajua Mziki Madee hajui laiti kama Dogo Janja angekuwa Mkubwa kama Madee basi Dogo Janja angekuwa Manager wa Madee kwa sababu Dogo Janja anajua Mziki ana Kipaji na ana uwezo wa kufanya Mziki na Ukafika Mbali na ndiyo maana Madee anaona Nisipokuwa na Dogo Janja Siwezi Kufika popote pale kwahiyo inamaana Madee Lazima Akae na Dogo Janja ili Dogo Janja aweze Kum Support Madee Afike Mbali hata kina Babu Tale Wanajua Kabisa Dogo Janja anajua Muziki kwahiyo Dogo Janja anapigwa Vita sana Mi Namkubali Dogo Janja na anajua Sina Beef na Dogo Janja na Namsupport na Nimefurahi Video aliyofanya Amefanya Classic na amewakazia Video yake ninayo na Nimemsaidia Kuisupport nimewapa Washkaji Huku Bahrain Wanaangalia ngoma ya Dogo Janja na inafanya Vizuri Kusema Kweli.
MADEE