NDOA YA MWIGIZAJI SHAMSA FORD YAVUNJIKA ‘DICK AMENINYANYASA NA KUNIPIGA KWA MUDA MREFU ILA NILIFICHA KUEPUKA AIBU”

Admin Updates10 years ago5 Views



Staa  mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford amefunguka rasmi kuhusu
kuvunjika kwa ndoa yake ya kimila aliyofunga na mwanaume wake wa siku
nyingi, Dickson ‘Dick’ akikiri kuwa amepoteza muda mwingi kwa mtu ambaye
hakuwa na mapenzi ya dhati kwake.

Akizungumza  na gazeti la Ijumaa Wikienda, Shamsa alitiririka kwamba
mara nyingi alikuwa akichezea kichapo tena akiwa na ujauzito wa miezi
minne wa mtoto wao, Terry lakini kipindi chote hicho alikuwa akivumilia
ili kukwepa aibu na kumlindia heshima.

“Dick ameninyanyasa kwa muda mrefu  lakini kuepuka aibu ya kuwa
mastaa hawatulii, nikawa navumilia kipigo kikali hivyo niliamua kuachana
naye tangu Oktoba, mwaka jana na sikutaka kusema ila sasa nimeweka wazi
kutokana na yeye kuanika mambo yetu kwenye mtandao wa kijamii,” alisema Shamsa.
Alipotafutwa Dick, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.