
Hili ni fundisho kwa vijana wengi ambao wanataabika, suala la fedha limekuwa mwiba mkubwa na chanzo kikubwa cha mahusiano na ndoa kuyumba. Nimelazimika nije na ushauri huu ambao utawasaidia vijana wa kileo ambao wanataabika na ndoa hususani suala la fedha.
Kinachowaumiza vijana wengi katika fedha na wenza wao ni tabia ya wanaume kuwa wazi kwa kutoa taarifa za pato lake kamili. Jambo la uwazi ni jema lakini muwe na kiasi kwani usipokuwa na akiba ya ‘taarifa za kipato chako’ utakosa fusra ya kufanya miujiza pale mambo yanapokwama.
Fanya hivi. Mfano kipato chako ni shilingi milioni moja kwa mwezi, mweleze kwamba unapokea shilingi laki 7 na hizo tatu hakikisha unaweka katika sehemu salama ambayo hata ikitokea umekufa familia yako itafaidika, mfano benki kila unapochukua mshahara hakikisha unaacha laki tatu kama akiba asiyoijua. Sasa katika hii laki saba panga matumizi pamoja na akiba ya pamoja.
Wanawake wanapenda ‘mshtuko/suprise’..so siku ya siku ukiona kanuna unamtoa shoping lazima ataona umetenda muujiza kwa nia njema. Hapa ndipo pale utasikia mwanamke anasema ‘mme wangu ana akili kweli’. Ikitokea una marupurupu fulani kama safari nk hakikisha unatoa kiasi na ziada unaweka chimbo. Hii itakupa upenyo wa kuwasaidia hata wazazi wako na ndugu zako bila kumhusisha mara kwa mara kwani wanawake wengine hawapendi usaidie ndugu na jamaa. Fanya mbinu hii hata kama kipato chako ni laki tano weka hata elfu hamsini chimbo ili uweze kutenda baadhi ya miujiza.
Wanawake wote duniani wamejaliwa karama ya kutumia hela yote ya mmewe, yaani ukimwambia kuna hela hii yeye ataandika orodha ya mahitaji ya familia ni kwani njema ila pesa zikiisha yeye hujitoa na kukulaumu kwanini ulitumia pesa zote. Yaani dharura ikitokea yeye hayupo ni lako hilo na ukishindwa kutatua hapo ndipo dharau inaanza…utasikia ‘mme wangu hana msaada kabisa’ yaani hajali kabisa matatizo anatumia pesa zote bila uangalifu.
Haya yote yanahitaji ustadi mkubwa na utimamu, kumbuka siku zote mwanaume anatakiwa kuwa mtu wa mshitukizo/surprise kwa kutumia kipato kile kile alichonacho. Yaani tunasema uwe na uwezo wa kutengeneza hela (money creator). Ikitokea dharura unamuangalia usoni huku ukitabasamu, unamwambia ‘mke wangu usihuzunike ngoja nifanye mpango nitatue hii shida’.
Hii ndio mbinu tuliitumia sisi na kuweza kuishi na mama/bibi zenu bila bugdha.
Nawakilisha.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






