Msanii Pofesa Jay Asimulia Mateso Aliyopitia Siku 462 ICU, Afichua Kutobolewa koo

Admin Updates1 year ago5 Views

 Nimepitia mengi katika siku 462 nilizokala kitandani, nimeona nimshukuru Mungu kwa ajili ya kipindi chote hicho na kunifanya niendelee kuwa hai hadi sasa na niwashukuru pia Watanzania kwa maombi na michango.

Hivi ndivyo anavyosema mwanamuziki Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay katika wimbo wake mpya alioupa jina la 462 ambaye amekuwa kwenye ugonjwa kwa takribani mwaka mmoja na miezi mitatu akisumbuliwa na figo.

Profesa Jay ambaye kwa sasa afya yake inaendelea kuimarika ameachia wimbo mpya unaoelezea maisha aliyopitia katika kipindi hicho cha ugonjwa kuanzia alivyoanza kuumwa hadi kupata nafuu.

Katika wimbo huo aliomshirikisha mwanamuziki wa injili Walter Chilambo, Profesa Jay ameimba akieleza hatua kwa hatua ya ugonjwa wake hadi kulazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi.

Baadhi ya mistari katika wimbo huo yamesikia akiimba, “Nilipumua kwa mashine hali ilikuwa mbaya, kila

kona ya mwili nikiwekewa mawaya. Moyo wangu ulisimama madaktari wakasema hauwezi kufanya kazi tena, mapafu yaliyaa maji, figo zikawa na mchanga nilishindwa kupumua kabisa na kutangatanga.

Nikaanza kufanyiwa dialysis na kutolewa sumu mwilini, nikawa napewa chakula kupitia puani wakawa wanavuta uchafu kupitia mpira kinywani, wakasema haisaidii inabidi wanitoboe koo sauti yangu ndiyo mtaji na ndugu wakasema no. Uchafu ukaongeza nikashindwa hadi kukohoa ndugu na madaktari wakakubaliana kunitoboa,”amerap Profesa Jay kwenye wimbo huo.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.