Katika hatua nyingine muimbaji huyo alizungumzia pia kuhusu nyumba yake.
Muimbaji
huyo amekuwa akipost picha ya nyumba yake hiyo yenye ghorofa moja na
kuwaacha watu wengi na maswali kibao ni wapi amepata uwezo wa kujenga
nyumba hiyo ilhali si msanii aliye busy na show kama wengine na hana
biashara kubwa anayoifanya kumwezesha kuwa na utajiri huo.
Hata
hivyo kupitia mahojiano na mtangazaji wa Kings FM, King Davidy, Jux
amesema nyumba ni ndoto aliyokuwa nayo hata kabla hajajulikana kwenye
muziki na hadi nyumba hiyo imefika hapo imetokana na desturi aliyokuwa
nayo ya kutunza fedha kwa miaka mingi.
“Watu hawawezi kujua mimi
nimeanza muda gani hadi kufika pale, unaweza kukuta hata miaka 10
iliyopita. Kwahiyo sio kitu cha jana na ni kitu cha taratibu, unapata
laki tano unaweka, unapata milioni mbili.. sababu nyumba haiozi kama
chakula, ni kitu ambacho kinaenda taratibu. Sio kama mimi tajiri sana na
nina hela, hizo ni dreams tu,” alisema muimbaji huyo.