
Rafiki huyo wa Johari alizidi kumwaga ubuyu kuwa katika kusaka faraja, staa huyo alijikuta amenasa katika mahaba ya mwanaume huyo na kuweka sawa mipango yote ikiwemo kutambulishana nyumbani na muda wowote watafunga ndoa.
“Ila naomba kabisa usinitaje, maana Johari hapendagi mambo yake binafsi yawe wazi, ana mwanaume wanayependana sana, ni mfanyakazi wa serikali.
“Wameshatambulishana hadi kwa wazazi, walikutana kipindi cha Johari akiwa na mawazo ya kuachwa na Ray, tena walikutana kwenye baa ya (akaitaja jina) pale Sinza, na kwa sasa Johari anafurahia mapenzi, jamaa mwenyewe anajulikana kwa jina la Martin,” alisema shosti huyo wa Johari.
Baada ya kumwagiwa ‘ubuyu’ huo, mwandishi wetu alichukua jukumu la ‘kusaga lami’ hadi ofisini kwa Johari, Sinza- Mori jijini Dar na kumtaka aweke bayana kuhusu penzi lake jipya ambapo alijibu kwa staili ya ‘kuingia na kutoka’.
“Aah, nani amekwambia habari hizo? Sipendi sana kuzungumzia mambo yangu binafsi sasa hata kama ni kweli kwani tatizo liko wapi? Mimi si mwanamke? Nilitarajia utaniuliza juu ya ujio wa filamu yangu ya True Love Never Die, wewe unakomalia mambo binafsi tu,” alisema Johari huku akiomba aachwe kwani alikuwa bize na kazi.