MPANGO WA KUMUUA DR. SLAA: MLINZI WAKE ALIPUKA….ADAI CHADEMA NI MAGAIDI……ASIMULIA JINSI ALIVYOTESWA NA KUPOTEZA NGUVU ZA KIUME

Admin Updates10 years ago4 Views

Siku
chache kupita baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando kufichua njama za Mlinzi wa
Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilbroad Slaa, bwana Khalid Kangezi kupanga
mipango ya kumuua  katibu huyo huku akishirikiana na Vigogo wa Chama
Mapinduzi CCM pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni,naye
Mlinzi huyo ameibuka  na   kufichua siri nzito ndani ya Chama hicho
kikuu cha upinzani nchini..



 


Akifichua
siri hiyo leo  mchana  Jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa
habari, Kangezi amesema amesikitishwa  sana na madai ya uongo
yanayoenezwa na viongozi wa CHADEMA  huku wakificha ukweli wa Mambo
kwani ukweli wa yeye kuzushiwa uongo huo unatokana na kuwa na mahusiano
na Mke wa Dr. Slaa .



 


“Nawashangaa
sana hawa Viongozi wa Chadema wanaosema mimi ni nimehusika katika
mipango ya kumuua Dr. Slaa. Wanaficha ukweli tu kwani sababu  ya
kuzushiwa uongo  huu inatokana na mimi kuwa na mahusiano mabaya na Mke
wa Slaa…

“Nilipoenda kumwabia Slaa, alisema niende
nikamalizane na  mke wake lakini ukweli ni kuwa mambo hayakwenda vizuri,
mke  wake  hakunielewa , ndipo  Slaa akapeleka  sakata  hilo  kwenye
uongozi wa juu” 
amesema kagenzi  na  kuongeza:



“Baada
ya Dr. Slaa kupeleka ugomvi huo kwenye ngazi za juu,juzi  wakati 
naenda  ofisini nilikamatwa na kupelekwa  chumba cha  mateso  kinacho 
milikiwa  na  Chama  hicho”



  

 Mlinzi Kagenzi akionyesha mateso aliyofanyiwa na  Makada wa Chadema


Bwana
Kagenzi ameendeleo kusema kuwa hata madai wanayodai kwamba anauhusiano
wa karibu na usalama wa Taifa pamoja na Vigogo wa CCM   ni ya uongo.



 


“Jamani
hivi inaingia akilini kweli mimi leo na maisha yangu haya niwe na
uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni uongo wa hali ya juu na
wanataka kunichafua kwa jamii tena niseme ukweli chama hiki kinataka
kuficha ukweli juu ya mambo waliyonitendea.



 


“Mimi
nimekuwa mlinzi wa Dr. slaa kwa muda wa miaka mingi sana ,tena nilikuwa
nampikia na kumtengea hadi chai ya kunywa eti leo niambiwe naandaa
mipango ya kumuua ? Huo ni unafiki”
 amesema Kagenzi



  

Akionyesha Vidonda


Mlinzi
huyo ameenda  mbali  zaidi  na  kufichua  mipango ya kigaidi
inayofanywa na Chadema huku akisema wameandaa ofisi  ya utesaji.



 


“Chama ambacho kinandoto ya kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia .
  
“Waliniteka
na kunifungia kwenye chumba cha mateso  wanachomiliki wao, wamenichoma
visu na kuniweka kwenye Mashine  ya umeme bila kosa lolote,eti
wakinishinikiza  nitaje wanaonituma. Jamani nawaambia  ukweli  na 
watanzania  wajue, situmwi  na  mtu  yeyote” .



 


Aidha, Kagenzi amekitupia lawama chama hicho na  kusema  kuwa  mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze nguvu za kiume .



  


Kuhusu
kuingiziwa Milioni saba kwenye simu yake na watu wa Usalama wa Taifa,
Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo  kwani hata simu yake haina
salio  na haijawahi kupokea pesa hizo. 



 


Kagenzi 
amehitimsha  kwa  kusema  kuwa baada  ya  mahojiano  na  jeshi  la 
polisi  sasa  anajipanga  kufungua  kesi  mahakamani  ili  kuwashitaki 
CHADEMA  kwa  mateso  waliyompa.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.