MLELA AWAPONGEZA WAANDAJI WA TAMASHA LA FILAMU “SZIFF”

Special Correspondent6 years ago6 Views

Na Khadija Seif, Globu ya jamii

MSANII wa filamu nchini, Yusuph Mlela amewapongeza waandaji wa tamasha la filamu za kitaifa    (SZIFF) kwa kuwapa fursa wasanii kujifunza kupitia masoko ya nje. Mlela ameeleza fursa waliyoipata katika mchakato wa tuzo ikiwa wazi kwamba bado wanafanya jitihada katika kuboresha na kukuza tasnia ya filamu nchini hasa kuonyesha filamu za nje na kukutanisha watu wanaofanya vizuri kutoka nchi za nje kutoa elimu kwa wasanii wa nchi zingine.

“Kuna utofauti mkubwa sana ukiangalia filamu za mataifa mengine na za kwetu hasa kwenye mtiririko wa matukio, ubora, uvaaji wa uhusiano, sisi bado tuko nyuma sana”. Alisema mlela

Hata hivyo amefafanua kupitia tamasha hilo tasnia itaimarika na kupanuka na kupata masoko ya nje na kujitangaza kwani sanaa ni ya watu wote, ni wakati wa wasanii kushirikiana kwa pamoja.

Aidha Mlela amesema kwa mwaka jana filamu ya kesho iliingia sokoni na kufanya vizuri  aliyomshirikisha msanii Gabo Zigamba na kwa mwaka huu kajipanga na vitu vizuri ambavo viko jikoni na kuwasihi mashabiki wakae mkao wa kushudia vitu vizuri.

Pia ametoa rai kwa waandaji wa Tuzo hizo kufanya kitu cha kipekee na tofauti katika kuboresha na kunogesha msimu huu wa pili japo ni changa kwa sasa, anaamini katika jambo lolote zuri lazima mawazo na maoni ni muhimu kuwasilishwa sehemu husika kufanyiwa ufumbuzi.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2ARbn6Q
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.