MISS TZ AMCHOKONOA ZARI KWA DIAMOND! WENYEWE WAFUNGUKA KIHIVI…

Admin Updates10 years ago7 Views


Musa mateja

Madai mazito! Mshiriki wa
Kinyang’anyiro cha Miss Tanzania 2011/12 ambaye alianza harakati za
kunyakua taji hilo akitokea Mkoa wa Shinyanga na baadaye kutwaa Taji la
Miss Kanda ya Ziwa, Glory Samwel anadaiwa kumchokonoa Zarinah Hassan
‘Zari The Boss Lady’ kwa kile kinachodaiwa kuwa ana ukaribu wa
‘kimalovee’ na mpenzi wa Zari, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa katika pozi na miss huyo. Chanzo cha
‘unyunyuzi’ huo kilitonya kwamba, mlimbwende huyo amekuwa akionekana
mara kwa mara akijivinjari na Diamond jambo ambalo wadau wamelishtukia
na kubaini kuwa ana mpango wa kuingilia penzi la Zari na kusambaratishia
uchumba wa wawili hao.
Ijumaa Wikienda lilinyetishiwa habari hizo
hivi karibuni na kuamua kuzifanyia kazi hatua kwa hatua, ambapo liliweza
kujiridhisha kwa baadhi ya matukio ya picha ambazo mrembo huyo amekuwa
akipiga na Diamond.
Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’. Mbali na picha pia kuna matukio ya sherehe za
‘bethidei’ ambazo Diamond alionekana akiwa karibu na mrembo huyo.

Ukiachilia mbali uchunguzi huo, mwanahabari wetu alimtafuta mrembo huyo
kwa lengo la kutaka kujiridhisha juu ya madai hayo ambapo alikiri kuwa
na ukaribu na Diamond huku akifafanua kwamba uhusiano wake na jamaa huyo
si wa kimapenzi kama wengi wanavyomchukulia.

“Hizo picha za
karibu zaidi ni zile ambazo tulipiga kwenye bethidei ya meneja wa
Diamond aitwaye Salaam, ambayo ilifanyika pale nyumbani kwake (Salaam)
Kijitonyama (Dar) hivi karibuni.
“Ni kweli watu wengi wananituhumu
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond lakini si kweli maana ninajuana
naye kawaida tu,” alisema Glory.

Kwa upande wa Diamond
aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa ni kweli anamfahamu Glory ila si mpenzi
wake na anachokijua ni shabiki wake kama ilivyo kwa wengine.
Alisema hata picha alizopiga naye hakuna picha za hovyo maana zilipigwa hadharani.
“Glory ni shabiki wangu wa kawaida tu kama ilivyo kwa mashabiki wangu
wengine, suala la kupiga naye picha halimaanishi ni demu wangu,” alisema
Diamond.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.