IMELDA MTEMA
MSANII
wa sinema za Kibongo, Brenda Malembeka ‘Kunguru’ ameibuka na kuanika
ukweli wa maisha yake kuwa kabla ya kutoka kisanaa, aliteseka sana kwa
kutumwa pombe na wasanii waliokuwa tayari na majina makubwa.
Msanii wa sinema za Kibongo, Brenda Malembeka ‘Kunguru’.
Akizungumza
na mwanahabari wetu, Kunguru alisema kwa kipindi hicho ilimlazimu
akubali kutumwa pombe na mastaa kwani lengo lake lilikuwa ni kupatiwa
nafasi ya kucheza uhusika ukuu. “Nilikubali sana kutumwa pombe na mastaa
wakubwa ili lengo langu litimie, nashukuru Mungu kwa sasa nimepata
shavu kwenye filamu inaitwa Asante iliyoandaliwa na Masai Media Group,”
alisema Kunguru.