Meneja wa Aisha Manula Afunguka Sakata la Manula na Simba “Tumesikitishwa Sana”

Admin Updates10 months ago6 Views

 

Anaandika Meneja wa nyanda wa Simba Sc, Aishi Manula, Jemedari Said Kazumari
✍️ “TUMESIKITIKA NA TUNAJIANDAA KULIPELEKA SUALA HILI MBELE YA MAMLAKA ZA MPIRA NDANI NA NJE YA NCHI.
Tunazungumza na wanasheria wetu kuona namna watakavyoshughulia suala la klabu ya Simba na mchezaji wetu AISHI MANULA kwa kitendo cha Simba KUMZUIA mchezaji kucheza soka ambacho kinapingana na kanuni za FIFA.
Mchezaji haumwi wala hana jeraha lolote, hajawahi kupewa taarifa yoyote na klabu yake ambayo ana mkataba nayo kwa mwaka 1, kuhusiana na chochote cha klabu.
Hajawahi kuambiwa kupima afya kwahiyo hajapima afya kama wengine, hajashirikishwa kwa namna yoyote kwenye mazoezi ya Misri mpaka timu imerudi hajaambiwa lolote na leo Simba imetangaza kikosi chake yeye hajatajwa popote mpaka Meneja wake alipolalamika ndiyo jina lake likatajwa.
Alipata timu ambayo iliandika barua kumuomba mchezaji lakini Simba wamekataa, wao hawamtaki na kumuacha aondoke akacheze hawataki pia, mchezaji maisha yake ni mpira na Simba wanamzuia mchezaji kucheza mpira, wanasheria watatuambia kanuni za FIFA zinasemaje na zile za TFF, zinaruhusu uhuni wa namna hii?
Mwisho Simba kama klabu inatoa meseji gani kwa wachezaji wengine? HAIKUBALIKI..!!”
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.