Mchambuzi Shaffih Dauda: Simba Bado Haijatoka Kwenye MBIO za Ubingwa, Acheni Kuongea Sana

Admin Updates1 year ago5 Views

 

Mchambuzi na Mdau wa Michezo Nchini Shaffih Dauda amesema timu ya Simba haijafanya vibaya kama ambavyo inazungumzwa, imetolewa kwenye Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ambayo imekuwa kikwazo kwao kwa misimu kadhaa mfululizo.
Kwenye makombe ya nyumbani imetolewa CRDB Bank Federation Cup hatua ya 16 bora, Simba tangu iliponyang’anywa kombe hili bado inapigana kulirudisha.
Simba bado inanafasi ya kuchukua Kombe la Ligi Kuu, hesabu za kwenye makaratasi bado zinakubali/zinaonesha nafasi ya Simba kuwa bingwa.
Hadi sasa Yanga ipo mbele ya Simba kwa alama tisa [9], timu hizo zinakutana Jumamosi kwenye mechi ya Ligi, Simba ikifanikiwa kushinda maana yake tofauti inabaki alama sita [6].
Simba ina mchezo mmoja wa kiporo dhidi ya Azam FC, ikiwa Simba itashinda mchezo huo maana yake inakuwa imeipunguza kasi Azam FC kwenye mbio za ubingwa lakini tofauti ya alama dhidi ya Yanga itakuwa imebaki tatu.
Kwa hiyo kwenye makaratasi Simba bado haijatoka kwenye mbio za ubingwa lakini ukiwasikiliza mashabiki tayari morali ipo chini na wamekata tamaa.
Mashabiki wa Simba wanapaswa kuwa waungwana na wanamichezo, kabla ya Yanga kuingia na kutawala soka la nyumbani wao walitawala kwa misimu minne mfululizo. Yanga kama watachukua msimu huu itakuwa ni mara yao ya tatu mfululizo kwa misimu ya hivi karibuni.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.