Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Tamrina Poshi ‘Amanda’.
Tujiunge na baadhi ya mastaa waliozungumzia ishu hiyo:Wasanii wa kike wengi ni malimbukeni kwani wakiona flani ana maendeleo na yupo na mwanaume flani wanammendea na kumchukua. Nina uhakika kutokana na tabia hii wengi tukienda kupima Ukimwi itakuwa ni hatari, hakuna atakayepona.Tabia hii ni ushamba pia kutokuwa waaminifu. Wapo wasanii walishawahi kunichukulia mwanaume wangu lakini siwezi kuwataja ila inakera sana. Kama ni ugonjwa wa Ukimwi basi utatuua wengi kwa sababu ya ushamba maana mtu akikuona uko na mtu wako anammendea wakati kabla hujawa naye walikuwa wanapishana tu.