MAPENZI/MAHUSIANO:MDADA ALIYEKWAMBIA KUJUA KUZUNGUSHA KIUNO NDO TIKETI YA KUPATA NDOA KAKUDANGANYA..

Admin Updates10 years ago7 Views


Kila
mwanamke anavitu vyake alivyojiwekea, ambavyo anataka mwanaume wa ndoto
zake awe navyo. Ikitokea akampata Mwenye hivyo vitu basi huona kamaliza
kila kitu, anajisahau, anafurahia vile anavyoviona kwa nje na
kitandani, badala aanze kumsoma huyo Mwanaume. Kama ni husband
material….


Wanawake
ndio wanaongoza kwa kulizwa Sana kwenye mahusiano kuliko wanaume,
kwasababu mwanamke akishampata mwanaume aliyekuwa anamtaka basi
atampenda kwa kila kitu, moyo na mwili wake wote kwa haraka wakati yeye
mwanaume hakupi vyote anakuangalia kwanza mpaka atakapoona kweli ndio
kitu anachokitaka ndio ataanza kukupenda kwa ukweli sasa. Lakini akiona
hakuna kitu atakuchukulia poa poa na baadaye anakupotezea, sasa wewe
uliyekufa na kuoza lazima upate ugonjwa wa moyo.


Mwanamke
usiende kwenye mahusiano kwa kuangalia picha ya nje, anza kwanza
kumwangalia Kama anaweza kuwa Mume na je unampenda kweli,
ukijihakikishia hapo anza kuwa wife material msaidie mwanaume hata kwa
mawazo tu sio unakaa tu kazi yako wewe ni kuzungusha kiuno tu.


Inatakiwa
ukiingia kwenye maisha ya mwanaume mwenyewe anakiri hakuna mwanamke
Kama wewe. Unambadilisha hata Kama hakuwa muoaji ajue umuhimu wa mke na
kutaka kukuoa

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...