MAPENZI:JITATHMINI KIMAPENZI KWA KUFANYA HAYA..BORESHA MAHUSIANO YAKO

Admin Updates10 years ago6 Views

Heri
ya Mwaka Mpya! Mimi na wewe tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha
kuumaliza salama mwaka 2014 na kuuanza mwaka mpya wa 2015. Najua wapo
wengi ambao walitamani kuuona mwaka huu lakini kwa namna moja au
nyingine, wakashindwa.


Karibu
tena tujadili mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi. Njia
nzuri ya kuuanza mwaka mpya, ni kupata muda wa kukaa na kutathmini
nyendo zako na mambo yote yaliyotokea katika maisha yako kwa kipindi cha
mwaka mzima wa 2014. 


Wengi
huwa wanakumbuka kujadili mambo yao ya kimaisha ikiwemo kazi, malezi ya
watoto, ujenzi wa nyumba, maendeleo ya biashara au vitu vinavyofanana
na hivyo lakini huwa wanashindwa kufanya tathmini ya jambo muhimu zaidi;
mapenzi na maisha ya ndoa.
 


Mipango
yako yote inategemea amani ya moyo na utulivu wa akili yako, huwezi
kuvipata vitu hivi kama utakuwa na migogoro ya mapenzi ndani ya ndoa au
uhusiano wako kila kukicha.
 


Kwa
kuzingatia hilo, ndiyo maana wataalam wa saikolojia ya mapenzi,
wanashauri kwamba wakati ukikaa na kutafakari mafanikio na matatizo
uliyokumbana nayo mwaka uliopita na kuandaa mikakati ya mwaka mpya, ni
muhimu sana kulitazama suala la mapenzi kwa upana wake.
 


1. ALIKUKOSEA NA WEWE UKAMKOSEA
Sisi
si malaika, kila binadamu hukosea na hakuna mtu ambaye ni mkamilifu kwa
asilimia 100. Yawezekana ukitafakari maisha uliyoishi na mwenzi wako
kwa kipindi cha mwaka mzima uliopita, unayaona makosa makubwa aliyowahi
kukufanyia. 


Hiyo
ni hatua ya kwanza lakini ya pili unapaswa kujitazama na wewe, lazima
yapo ambayo ulimkosea na pengine kusababisha kulegalega kwa mapenzi
yenu. Unapouanza mwaka mpya, ni muhimu sana kukaa na mwenzi wako na kwa
pamoja mkajadili mambo mliyokoseana kwa lengo la kuyamaliza na kufungua
ukurasa mpya.
 


Tafuta
muda ambao nyote mtakuwa mmetulia, kila mmoja aeleze dukuduku lake na
makosa aliyowahi kutendewa na mwenzake kisha kubalianeni kuweka pembeni
tofauti zote za mwaka uliopita na kuangalia mwaka mpya.
 


2. UMETIMIZA AHADI KWA KIWANGO GANI?
Lazima
zipo ahadi ambazo ulimuahidi mwenzi wako, na yeye lazima zipo ahadi
ambazo alikuahidi. Mnapoanza mwaka mpya, ni wakati wa kila mmoja
kutathmini jinsi alivyotimiza ahadi alizomuahidi mwenzi wake. 


Wahenga
wanasema ahadi ni deni, hakuna kitu kibaya kama kumuahidi mwenzi wako
jambo halafu ukashindwa kulitimiza bila kuwa na maelezo yoyote. Hebu
orodhesha ahadi zote ambazo uliwahi kumpa na jiulize umezitimiza kwa
kiwango gani? 


Ukigundua
ahadi nyingi zimekuwa hewa, ni wakati wa wewe kuzungumza na mwenzi wako
kabla hata hajakukumbusha. Mueleze nini kilisababisha ukashindwa
kutimiza ulichomuahidi, hiyo itamfanya aone kwamba wewe ni mtu
unayejali, atauanza mwaka vizuri akiwa na uhakika kwamba yupo na mtu
makini. 


3. UMEMSALITI MARA NGAPI?
Nilisema
na nitaendelea kusema kwamba hakuna kitu kibaya kama usaliti. Wakati
ukiuanza mwaka mpya, jiulize mwenyewe ndani ya moyo wako; ulimsaliti
mwenzi wako mara ngapi? Yawezekana mwenyewe hajui lakini ndani ya moyo
wako unao ukweli. 


Kama
hujawahi kumsaliti, una haki ya kujipongeza na kuendelea na moyo huohuo
kwani uaminifu ndiyo nguzo kuu ya mapenzi. Hata hivyo, kama unajua
kwamba umesaliti mara kadhaa, zungumza na moyo wako mwenyewe na jiahidi
kwamba hutamsaliti tena na tekeleza ahadi hiyo kwa vitendo, bila kujali
vishawishi unavyokutana navyo.

Tukutane wiki ijayo kwa mwendelezo wa mada hii. Kwa maoni, ushauri, nicheki kwa namba za hapo juu.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.