MAPENZI:HIZI NDIZO ATHARI ZA KURUHUSU MUMEO AFANYIWE MASAJI NA MWANAMKE MWENZIO… HIZI HAPA..

Admin Updates10 years ago7 Views


Inabidi sasa wanawake tuanze kuwapa somo wenyewe manake inaonekana hamfundishani kabisa. Sababu kila kukicha Mambo ni yale yale.

Wanawake
mmekuwa na tabia mume akikueleza anajisikia vibaya,mwili unamuuma
haraka unamwambia nenda hospitali au unakwenda kumnunulia panadol
apunguze maumivu, Mnakosea kabisa.


Kumbe
daktari au nesi au mtabibu ni wewe mwenyewe, hebu nikupe siri moja wala
usiniulize mchaichai nitaupata wapi, kwani uko mwingi sokoni na kwenye
maduka ya dawa za asili. Chukua nazi zako, zikune halafu chuja taratibu
mpaka upate tui zito, pika mafuta ya nazi, ule muda ambao tui lako liko
jikoni chukua majani ya mchaichai changanya kwenye tui hilo wakati
linachemka changanya na mdalasini pamoja na hiriki, acha tui lichemke
mpaka ligande. Likishaganda unatoa mafuta mazuri yanayonukia kisha chuja
na uweke kwenye chupa safi.

Muinue
mumeo kamuogeshe, ikiwezekana hata kumbeba mbebe, mwanaume si mzito
hata akiwa na uzito wa tani tano huwezi kushindwa kumbeba,mbona mkiwa
kwenye mahaba uzito huuoni? Mume anafanyiwa kila linalowezekana ilimradi
liwe halali kwa Mwenyezi Mungu. Mwanaume ni bahati, hawapatikani
kilahisi. Hakikisha mume unamshikilia asikuponyoke. Siku hizi wanaume
tumekua adimu hadi tunagombaniwa, walio na moyo mwepesi wanajichoma visu
wengine wanakunywa sumu, unabaki unajiuliza kwani anayo ya dhahabu?
Mwanaume ni zawadi kutoka kwa Mungu. Na siri ya tungi aijuaye kata.

Sasa
mbebe mumeo kisha kamuogeshe na baada ya hapo mkaushe kwa taulo laini
siyo kwa kanga na usimsugue, taulo lina manyoya yake ambayo ni malaini
na ni maalum kwa ajili ya kufutia maji, kanga inasugua ngozi si salama
sana pia kwa sababu inatoa rangi.

Baada
ya kukausha maji chukua mafuta yako umpake mwili mzima kisha fanya
masaji taratibu, baadhi ya wanawake wanawapeleka waume zao kwenye vituo
vya masaji wakafanyiwe masaji ya mwili, hivi kwa nini mumeo
akashikweshikwe na mwanamke mwenzako wakati ufundi wewe unao?
Kama huna ndiyo huu nakupa.

Mpapase
taratibu mumeo huku unamfanyia masaji, fika mpaka kwenye milima ya
gorani, teremka taratibu kwenye bonde la Sinai, hapo sasa utakapofika
kwenye bonde hilo sidhani kama maumivu yatakuwepo, lazima atataka
chakula cha usiku hata kama itakuwa mchana atataka cha usiku tu Mlishe
usimnyime chakula. Mimi nawasaidia Mahusiano yasiwashinde. Unashangaa
mwenzio anadumu kwenye mahusiano unaanza kusema kaenda kwa mganga kumbe
hujui anayo mfanyia Mpenzie. Chukua hatua.
 

Watakucheka
watu ukiachwa, Mara Nyingi Huko Kwenye Vituo vya masaje Mwanaume akiwa
anafanyiwa hiyo masaje na Mwanamke ikilolea atataka na papucha ..Shauri
Zenu

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...