MAONI:UNAMSHAURI NINI AUNT EZEKIEL KUHUSU UGOMVI NA WEMA?

Admin Updates10 years ago4 Views



Kwa kuangalia historia ya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel ni zaidi ya
marafiki ambao walikuwa maswahiba walioshibana kiasi kwamba hakuna mtu
anaeweza kujua kama leo watakuwa maadui. Na urafiki huu ulikomaa zaidi
pale Madame Wema alipokuwa amerudiana na Diamond Platinumz kiasi kwamba
hata safari za nje za Wema na Diamond na Aunt nae alikuwa anasafiri na
hatukujua alikuwa anasafiri kwa gharama ya nani.

Kwa ukaribu huu wa Wema na Diamond kulimfanya Dogo wetu Moses Iyobo
kupata bahati ya mtende kilaini kwa dada yetu Aunt Ezekiel ambaye
walianza mapenzi chini chini na kuficha kila walipoulizwa kama wana
uhusiano ila alikataa, ila mwisho ya yote yalikuja julikana baada ya
Aunt Ezekiel kupata ujauzito.

Sasa ikawa hawana jinsi lazima waweke wazi. Hatujui kama Madame Wema au
Diamond alitumika kupiga pande kwa hawa wapenzi wawili ama la ila chanzo
ni yeye kuwa na ukaribu na Diamond na Aunt Ezekiel ndo kukampa mwanya
Moses Iyobo nae kuwa na uhusiano na Aunt Ezekiel.

Sasa leo kuna kamtihani kamemkuta Aunt Ezekiel kwa kuwa Madame Wema
ameachana na Diamond Platinumz, na kuachana kwao kumetengeneza mgongano
mpaka kupelekea kuwa na Team Diamond& Zari na Team Wema. Kwa
kuangalia kwa umakini zaidi Aunt Ezekiel anakaribia kupata mtoto na
Moses Iyobo na Upande mwingine bado yuko na Uswahiba na Wema Sepetu.

Aunt Ezekiel anapata mtihani kwa kulazimishwa na Wema kuwa bado awe
kwenye Team Wema wakati yeye tayari ana usiano na Moses Iyobo ambaye ni
Dancer wa Diamond na ukiangalia kwa umakini kila itakavyokuwa lazima
Moses ndo anauhusika na kila kitu kwa huduma za Aunt Ezekiel.

Sasa ukiangalia kwa mbali kuna ugomvi wa chini chini kati ya Wema na
Aunt Ezekiel ikisemekana kama Wema hataki Aunt Ezekiel amsapoti Diamond
ila naamini Aunt Ezekiel anafanya ivi kwa mapenzi ya mpenzi wake Moses
Iyobo.

Ukiwa kama wewe mdau unaweza mshauri nini Aunt Ezekiel;

1- Aaache kumsaport Diamond kwa kulinda urafiki wake na Wema?

2- Aache kumsaport Wema ali ajenge uhusiano zaidi na Moses Iyobo na kwa faida ya mtoto wao?

3- Au afanya uamuzi gani kwa hawa wahasimu wawili ili aweke mambo sawa kwa pande zote mbili.

Tumshauri dada yetu please bila matusi.

By Abatmwe on JF

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.