Udaku Special Blog: SIKU chache baada ya kuvuja kwa picha
zinazomuonesha mpenzi wa sasa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan
‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo kinachoashiria kukua kwa ujauzito,
mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu
amefunguka kuwa amefurahia tukio hilo.
Mzazi huyo ambaye ni fundi wa kuzungumza, alisema tukio hilo
limemfurahisha kwani anaamini ndoto za Diamond kurudiana na binti yake
zitakuwa zimeyeyuka rasmi kama alivyokuwa akimuomba Mungu siku zote.
Kuonesha kwamba amefurahishwa na kitendo hicho, alimtaka Zari aendelee
kumpenda Diamond, amgande kila idara ili isije kutokea akarudi kwa binti
yake ambaye walimwagana mwishoni mwa mwaka jana.
“Yaani kama inawezekana naomba sana huyo Zari azidi kumganda Diamond,
asimpe muda wa kugeuka nyuma kabisa ili mambo mengine yaendelee kwa
sababu uhusiano wa Diamond na mwanangu haukuwa na baraka zangu,” alisema
mama Wema.
Mama Sepetu aliongeza kuwa, hana maana ya kumchagulia mchumba mwanaye
bali anahitaji mwanaume yeyote mwenye heshima na anayehiheshimu kwa
sababu mwanaume asiyejitambua hawezi kuwa baba bora wa familia.
“Sio kwamba namchagulia mtoto wangu mume gani amuoe lakini nahitaji mtu
mwenye heshima na kujiheshimu mwenyewe ndio anaweza kuwa baba wa familia
la sivyo inakuwa ni mambo ya kihunihuni tu kama ilivyokuwa kwa
Diamond.”
Alipotafutwa Diamond kuhusiana na kauli hiyo ya mama Wema, simu yake
iliita bila kupokelewa lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram, staa
huyo wa Wimbo wa Mdogomdogo, alitupia picha ya Zari huku akizungushia
duara tumboni na kuandika; ‘kileee kinaanza kumharibia mtu mavazi.’
~Stori: Imelda Mtema/Amani