KWENU
wasanii wa Bongo Movies. Bila shaka mko poa na mnaendelea na
mishemishe zenu za mjini kama kawaida. Kutokana na ubize wa kazi zenu
na zangu, leo nimeona bora niwakumbuke kwa barua.
Mkitaka kujua hali yangu, mimi ni
mzima wa afya namshukuru Mungu naendelea na majukumu yangu kama kawaida
ambapo moja ya majukumu hayo, ni hili la kuwaandikia barua
kuwakumbusha pale ninapoona hamuendi sawa au kuwapongeza mnapofanya
vizuri.
Dhumuni la barua hii ni kutaka kuwauliza ni nani
amewaroga? Imefika hatua nimeona niwaulize swali hilo kutokana na
mustakabali mzima wa mvuto wa sanaa yenu uliopo kwa sasa.Kutokana na
kazi yangu, mbali ya kufanya kwa ukaribu na makundi mengine ya
kijamii, nimefanya na nyinyi kwa muda mrefu kidogo, najua baadhi
yenu mtakuwa ni mashahidi wa hili.
Pointi yangu hapa ni hii.
Kuna wakati nyinyi wasanii wa filamu mlikuwa juu sana kimauzo,
umaarufu na hata mafanikio kwa jumla. Mlikuwa ndiyo mnaozungumzwa
mitaani na kila rika. Si watoto, mama na hata baba zao. Sinema
zilikuwa !٪zinakamata!& watu kwelikweli.
Si mnakumbuka
kipindi kile mlivyokuwa mnaonekana nyinyi tu hata katika muziki wa
bendi, watakuwepo mastaa wengi ukumbini lakini utasikia majina ya
wasanii wa Bongo Movies !٪yakirushwa!& ukumbini. Mitaani
kwenye !٪vibanda-umiza!& ilikuwa kila mmoja anazungumzia
mastaa wa sinema pengine kuliko mastaa wa muziki, wanasiasa na hata
wanamichezo. Lakini kwa takriban miaka mitatu iliyopita ufalme wenu
umepokwa na Bongo Fleva.
Sasa hivi watoto wanamjua Diamond, Ali
Kiba na wengineo lakini si nyinyi tena. Wanafuatilia kazi zao,
wanafuatilia habari zao. Wanataka kujua wanafanya nini katika maisha
yao ya sanaa kila siku. Mafanikio ya wasanii wa muziki yanaonekana
dhahiri. Mashabiki wanaona wanavyovuka mipaka, wanaona wanafanya
shoo na kutengeneza mamilioni katika nchi za watu.
Upande wenu
kimya kimetawala. Si kwamba hamtoi muvi, la hasha. Mnatoa lakini
mvuto umepungua. Watu hawazifuatilii sababu mvuto wenu umeshuka.
Sinema mnazitoa, Wabongo hawaoni zile mishemishe za nyinyi kutangaza
kazi mpya, kufanya matamasha makubwa ya sinema, kuvuka mipaka ya
Tanzania hata kwa kufanya ziara katika nchi za jirani kama ilivyokuwa
kipindi kile cha kina Vincent Kigosi !٪Ray!&, Steven
Kanumba (marehemu) na wengineo.
Ndugu zangu mbona mliweza
kipindi kile halafu sasa mshindwe? Hata kama mnashindwa kwenda kwa
pamoja jitihada binafsi zinahitajika. Pigeni kazi za
!٪individual,!& vukeni mipaka kwa nguvu zenu tuone
mnatoboa.
Msikae mbali na vyombo vya habari, mnajiharibia
wenyewe bila kujijua. Fanyeni kazi, zifikisheni kwenye media kazi
zenu zitangazwe na si kuweka chuki na waandishi halafu baadaye mnakuja
kulaumu kwamba mnatengwa.
Najua mnaweza, naamini mnaweza kuamka
na kufanya mambo makubwa ya kushangaza. Fanyeni kweli na sisi tutawapa
sapoti! Kutakapokucha