MAJANGAA:MPENZI WA FACEBOOK AFANYA MAUAJI KWA KUMNYONGA MKE WA MTU GESTI HOUSE

Admin Updates10 years ago6 Views

KWELI mchepuko siyo dili! Kauli hii imedhihirika kufuatia mwanadada,
Ashura Maulid, mkazi wa Ilala jijini Dar, kukumbwa na mauti kwa madai ya
kunyongwa ndani ya gesti na mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la
Charles ambaye inasemekana ni mpenzi waliyekutana kwenye mtandao wa
kijamaii wa Facebook.

Tukio hilo lililojaa majonzi tele na kuacha maswali mengi, hasa kwa mume
wa marehemu, Suleiman Othman, lilijiri  Mei 19, mwaka huu kwenye nyumba
ya kulala wageni (jina lipo) iliyopo kandokando ya barabara ya kutoka
Sinza Afrikasana kwenda Kijitonyama kupitia Kituo cha Polisi cha
‘Mabatini’, Dar.

Chanzo kinadai kuwa, enzi za uhai wake, mwanadada huyo alikuwa
akijihusisha na biashara ya kuuza duka la friji maeneo ya Sinza ya
Afrikasana na inasemekana amekuwa ndani ya ndoa na mumewe, Suleiman kwa
miaka 15 na kujaliwa kupata watoto wawili, wa mwisho akiwa na umri wa
mwaka mmoja na nusu.

Akizungumza na Uwazi, Ijumaa iliyopita huku akiwa katika majonzi mazito,
mume huyo alisema Jumanne ya Mei 19, mwaka huu, mkewe alimuaga
anakwenda kazini huku akiumwa, alimtaka apumzike lakini mwanamke huyo
akasema anajiona amepona hivyo ana uwezo wa kumudu majukumu yake.

Ilipofika saa moja usiku akanitaarifu kuwa ameshatoka kazini. Cha
ajabu mpaka saa nne usiku alikuwa hajafika nyumbani na nilipompigia simu
hakupokea.“Mara kwa mara mke wangu alipokuwa akimaliza kazi na kuanza
safari ya kurudi nyumbani alikuwa ananitaarifu, nachati naye kila wakati
mpaka anafika. Siku hiyo nilikuwa nina majukumu mengi aliponitaarifu
kamaliza kazi ndo’ anarudi sikuwa na presha.



“Sasa ilipofika saa nne mimi nikiwa nyumbani na simu hapokei,
nikashangaa. Mbaya zaidi, baadaye simu yake ikawa haipatikani
kabisa.“Nilifanya jitihada za kumtafuta kwa ndugu na jamaa, vituo vya
polisi na hospitali mbalimbali, ikiwemo Muhimbili kuulizia kwenye wodi
za wagonjwa lakini sikumkuta.

Juzi (Mei 20), nilishtuka kupigiwa simu na polisi wa Kijitonyama,
wakaniambia kuna maiti imekutwa mahali (walimficha kama ilikuwa gesti)
na aliyehusika na mauaji ni mwanaume ambaye walianza kufahamiana na mke
wangu kupitia Facebook. Walisema marehemu alionekana alikufa kwa
kunyongwa.



“Waliniambia huyo mwanaume alikimbia baada ya kufanya mauaji hayo.
Palepale ndo’ wakaanza jitihada za kumtafuta mpaka wakamkamata,” alisema
mume huyo.Akiendelea kuelezea tukio hilo alisema kisa cha kugundua kuwa
Charles alikutana na mke wake kwenye Facebook ni siku ya tukio baada ya
mawasiliano waliyoyafanya kwa kipindi kirefu bila yeye kujua
.

Alisema ilionesha kuwa, siku hiyo waliamua kuonana laivu ambapo
alimkaribisha dukani kwake na kuondoka naye baada ya kumaliza kazi na
kufunga duka huku akiwa amemtaarifu bosi wake (si mumewe) fedha
zilizopatikana siku hiyo.
“Niliambiwa na rafiki wa mke wangu kuwa siku hiyo mwanaume huyo alifika
dukani kwa mke wangu akawatambulisha mashosti zake kuwa ni rafiki yake
waliyejuana Facebook. Wakiwa hapo, mke wangu  alimpigia simu bosi wake
kumwambia siku hiyo aliingiza shilingi milioni moja na laki saba. Huenda
hicho ndo’ kilimfanya jamaa amgeuke na kumuua kwa tamaa ya zile fedha,”
aliongeza.

Mumewe huyo alisema, haamini kama mkewe alishindwa kuiheshimu ndoa yake
na kuwapa nafasi wanaume wengine tena kwa kwa mtu ambaye hakufahamiana
naye ila kwa kukutana naye kwenye mtandao na kuanzisha uhusiano kwani
yeye alimtosheleza kwa kila jambo.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura
alipotafutwa ili aulizwe kuhusiana na tukio hilo, simu yake iliita bila
kupokelewa.Uwazi lilipofika kwenye gesti hiyo ambayo marehemu alifia
chumba Namba 4 lakini wahusika  waligoma kutoa ushirikiano na kudai
hakukuwa na tukio hilo.

Kesi  hiyo ipo katika Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ faili
Namba KJN/RB/5081/15 TAARIFA YA KIFO huku mtuhumiwa akishikiliwa hapo
baada ya kukamatwa akiwa na gari aina ya Toyota Carina

GPL

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.