MAHUSIANO: ISHU SI KUOA, ILA UNAMUOA NANI KWA VIGEZO GANI??? ..ENDELEA HAPA MWENYEWE UJUE

Admin Updates10 years ago5 Views


Kwa
moyo mkunjufu nikukaribishe mpenzi msomaji wa safu hii ya Love and
Story, tunapata kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo maisha ya uhusiano.


Kwa
wale tulioianza mada ya ishu siyo kuoa, ila unamuoa nani kwa vigezo
gani wiki iliyopita, hakika wataungana nami kwamba ili uishi usije
kujutia ndoa yako, yakupasa kuchagua mke au mume sahihi.

Tunaimalizia mada hii ambapo hakika itakuwa ni funzo kwa pande zote mbili, mwanaume na mwanamke.

Kwenye ndoa kuna wakati wa maradhi. Yawezekana ukaumwa wewe au
akaumwa hata ndugu yako, je mkeo atakuwa tayari kukuhudumia. Mbaya zaidi
ugonjwa wenyewe unaweza kuwa wa kutia kinyaa, atakuwa tayari
kukuhudumia au kuwahudumia ndugu zako?


Lazima ujue kwamba anaweza kustahimili katika hali kama hiyo au
maneno yale ya kwamba; “mtaishi kwa shida na raha” yeye atayageuza na
kuwa tayari kwa maisha ya raha tu, ya shida hayawezi.

Asiwe mtu wa kwenda na wakati asiyetaka hata kucha zake zisiingie maji kwa kuosha vyombo. Hajui kufua nguo.

Asije kuwa yule wa kufanyiwa kila kitu na dada wa kazi. Yeye ni mtu
wa kuelekeza kila kitu halafu dada afanye, suala la kupika kwake ni
kizungumkuti.


Mwanamke wa aina hiyo hafai kuwa mama wa watoto. Unafikiri atawafundisha nini wanaye? Ujinga tu!

Mke ndiyo msiri wako, ndiye ambaye anaweza kukushauri kitu pale fikra
zako zinapokutana na vikwazo. Siku hazifanani, leo waweza kuwa vizuri
lakini kuna siku unaweza kuwa na mawazo, hapo ndipo anapopaswa kutumia
nafasi yake kama mke kukurudisha katika hali ya kawaida.


Marafiki
zangu, tukubaliane tu kwamba mkeo ndiye mtu pekee ambaye unatumia muda
mwingi zaidi kuwa naye karibu. Utakuwa kazini ambako mnashirikiana na
wafanyakazi wenzako kwa saa kadhaa  lakini utarudi nyumbani ambako
utatumia muda mwingi zaidi kuwa na mwenzako.


Hivyo basi asipokuwa mtu sahihi kwako ni dhahiri kwamba atakuangusha.
Lazima uwe na mke ambaye anawaza maendeleo awe anajua anapaswa kufanya
nini pindi tatizo linapotokea, asijekuwa mtu wa kulikimbia tatizo.


Awe mvumilivu katika kipindi ambacho uchumi utayumba ndani ya nyumba.
Ajue kwamba wewe ndiye mumewe katika hali yoyote. Asije akawa mwepesi
kukusaliti kwa sababu tu ameona mpo katika kipindi kibaya kiuchumi.


Badala ya kukusaliti au kukukimbia, anapaswa kufikiri zaidi juu ya
mbinu mbalimbali za kujinasua katika tatizo linalowakabili. Badala ya
kukaa kusubiri kuletewa kila kitu basi pengine na yeye aweze kubuni
miradi midogomidogo ambayo inaweza kupunguza makali ya ugumu wa maisha.


Elimu hii si ya wanaume pekee, wanawake nao wanapaswa kuitumia ili
kuweza kujua sifa za mwanaume ambaye anafaa kuwa mumewe. Usikurupuke
kuolewa na mtu ambaye huna imani naye au kwa kigezo kwamba pengine ana
uwezo wa kifedha.


Lazima ujue ni mtu ambaye anaweza kustahimili shida na raha. Atakuwa
bega kwa bega pale wewe utakapohitaji msaada wake? Vinginevyo usikubali,
mpe muda wa kutosha kumjua tabia yake. Kama kuna kitu unaona hakipo
sawa na kinaweza kurekebishika basi jaribu kumshauri na ukiona hawezi
basi ni vyema ukaachana naye usije kujuta baadaye.


Kila mmoja wenu anapaswa kuoa au kuolewa na mtu ambaye anakidhi na
hali ya aina yoyote. Ndoa si lelemama, haina majaribio, mkikubaliana
basi hakuna kugeuka nyuma!
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.