MAHABA:MWANAMKE WATANGULIE WAMBEA MAPEMA KABISAA, ILI WAKIJA KUMNONG’ONEZA AWAAMBIE, ‘NINAJUA’

Admin Updates10 years ago7 Views



Hebu nikuulize wewe mwanamke. Je umewahi kumficha mumeo au mpenzi wako
kitu chochote kuhusu maisha yako ya zamani au ya sasa? Je mumeo au
mpenzi wako ameshawahi kukushangaza na siri ya mambo yake ya
zamani?Inawezekana jibu likawa ndiyo au hapana, lakini kuanzia leo
ningependa ujifunze jambo moja kwamba ni siri gani unatakiwakuzitoa na
ni siri gani hutakiwi kuzitoa. Usijidanganye kwamba unaweza kuficha kila
siri, lakini usijiamini kwamba kwa sababu unaitwa ‘honey’ ukitoa kila
siri utaweza kunyoosha uhusiano wenu, thubutuu…………….!Lengo la kuficha
jambo ni kwa ajili ya kujilinda. Unaweza kudhani kwamba, kwa kusema siri
zako za zamani za masuala yako ya mapenzi utaonekana shujaa utaonekana
mwadilifu au utaonekana mcha Mungu. Hapana, kuna wakati kusema kila
jambo, kunakufanya ushindwe kujilinda na kumlinda mwenzi wako.Kuna mambo
ambayo huna budi kuyatoa, kama siri uliyonayo inaweza kuyumbisha
mustakabali wa uhusiano wenu au kuweza kuvunja ndoa yenu. Mtaalamu wa
uhusiano na mtunzi wa kitabu cha Is He Mr. Right? Mira Kirshenbaum,
anasema, hata mambo ya zamani ambayo yanawezakuleta athari katika
uhusiano au maisha ya ndoa (madeni sugu, magonjwa ya kurithi, wapenzi wa
zamani, tabia mbaya ambazo ulikuwa ukifanya zamani) inabidi visemwe,
kutegemea tu nafasi kama vitakuja kufahamika au la. Lakini kumbuka,kama
jambo linafahamika kwa zaidi ya mtu mmoja, siyo siri, litakuja kumfikia
mwenzio tu.Kuna wakati wanandoa wanaona kama wamechelewa kutoa siri na
hivyo hunyamaza na baadae siri inapofichuka watu wanaanza
kuchanganyikiwa. Lakini ukweli ni kutojua tu, pale unapokumbuka siri,
ambayo una uhakika itafahamika kwa mwenzio, iseme, usisubiri. Tatizo la
siri, ni kuwa huwa inaumiza sana. Kwa binadamuwengi kufuta uongo au
usaliti siyo jambo rahisi.Mtu aliyefichwa siri anajiona kwamba
alisalitiwa, kwa hiyo hujenga chuki kubwa.Hata kama unaona siri yako ni
kuhusu jambo dogo kwako, tafadhali usimfiche mwenzio. Kama ukweli wa
jambo hilo utakuja kujulikana baadae, madhara yanaweza kuwa mabaya zaidi
kuliko kama ungekuwa umemwambia mapema. Sio kwamba mwenzi wako
anahitaji kupata habari ili mshirikiane kutatua jambo lililo mbele yenu,
lakini pia anahitaji kwa ajili ya kujua kama unamwamini.Ipo kanuni moja
kuhusu mapenzi inasemaunavyozidi kutotaka kuitoa siri ndivyo
unavyoiombea ijitokeze ghafla na kuanikwa hadharani. Vipi kuhusu mpenzi
wako wa zamani kwamba anaweza akajitokeza ghafla ikajulikana kwa mumeo?
Kama unahisi kwamba mwenzi wako anaweza kuja kupata habari za mpenzi
huyo wa zamani, basi hakikisha kwamba unamweleza kabla
hajatambua.Kujisafisha na wapenzi wako wa zamani nijambo zuri. Bali
jaribu kuwa mwangalifu, silazima katika maelezo yako ukaanza kumsimulia
mwenzio hata u.pu.u.z.i mliokuwa mkifanya wakati wa mapenzi yenu. Ni
wajinga tu ndio wanaofanya hivyo.Wenye hekima husema tu ukweli
kwamba,waliwahi kuwa na uhusiano na huyu au yule na fulani na fulani.
Hata kama ni kumi,wataje, ili mwenzio aamue mwenyewe, usijidanganye
kwamba, hatakuja kujua. Watangulie wambea mapema kabisaa, ili wakija
kumnong’oneza awaambie, ‘ninajua’Wapo wanawake wengine huyumbisha
uhusiano na weza wao au ndoa zao kwa kufukunyua mambo madogo madogo. Si
vyema sana kuleta udadisi kwenye mambo madogo madogo ambayo hata hayana
maana wakati mwingine. Usimsumbue mwenzio kutokana na gharama ya simu au
kamera yake, hasa kama na wewe hutaki akuulize kuhusu bei ya mkoba au
kidani chako…
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.