Hawataki
kuwa viruka njia, wanataka waipate ile raha ya ndoa, raha ya kuitwa mke
wa mtu lakini pia wengine wanataka waingie kwenye ndoa ili
wazae.Kimsingi kuna utitiri wa wanawake wanaotaka kuolewa huko mtaani
lakini wanaume wengi ambao wako kwenye umri wa kuoa wanadai bado wapo
wapo kwanza.
Wanasema
wanawake wa kuoa hawajawaona, wanahisi wakiingia kwenye ndoa wataumizwa
eti kwa sababu usanii umekuwa ni mwingi kwenye mapenzi.Hata hivyo, wapo
wanaume wengi ambao wanahangaika kutafuta wachumba. Si kwamba wasichana
wa kuoa hawapo, wapo lakini tatizo ni kumpata yule mwenye vigezo vya
kuitwa mke ‘wife material’. Sasa, leo nataka kuwapa msaada wanaume ambao
wanahangaika huku na kule kumbaini mwanamke mwenye sifa ya kuitwa mke.
ANGALIZO
Kuna
wanawake ambao ni wajanja sana, wanaweza kujivisha ngozi ya mbuzi kumbe
ndani ni chui. Wana uwezo mkubwa sana wa kuficha makucha yao lakini
wakiingia kwenye ndoa utashangaa namna watakavyoyatoa na kukufanya
ujute.
Kwa
maana hiyo basi, kama unatafuta mke kwa maana halisi ya mke, unatakiwa
kutumia muda mrefu sana kumchunguza huyo ambaye unahisi anaweza kuwa
mama wa watoto wako.
SIFA ZA MWANAMKE ‘WIFE MATERIAL’
Anayejua kuna shida na raha
Wapo
wanawake ambao wao wanajua kila siku ni Ijumaa, yaani hawatambui kwamba
kuna Jumamosi na Jumapili pia. Watu hawa ni wale wanaodhani maisha ni
raha tupu na kwamba wanaoishi kwenye shida ni wajinga.Ukweli hauko
hivyo, maisha yana changamoto nyingi sana. Kuna siku mambo yanaweza kuwa
si mazuri lakini siku nyingine mambo yakawa supa. Mwanamke wa kuoa
lazima ajue hivyo.
Hana tamaa za pesa
Katika
maisha ya sasa mwanamke anayependa sana pesa ukikubali awe mkeo
mtasumbuana sana. Kwa maana hiyo mwanamke ambaye utagundua hana tamaa ya
pesa, kwamba ikiwepo, ikikosekana anabaki kuwa yeye, huyu ni ‘wife
material’.

Hayuko tayari kukuona huna amani
Mwanamke
ambaye unaona kabisa unapokuwa na matatizo anaumia, anahaha kuhakikisha
anakurudisha kwenye hali ya kawaida, huyo anafaa kuwa mkeo.
Anapenda watoto
Utajuaje
kama ana mapenzi na watoto? Iko hivi; katika uhusiano wenu ukiona ni
mtu wa kupendapenda sana watoto wa marafiki zake, kuwanunulia zawadi,
kuwashauri wenzake namna nzuri ya kuwalea watoto, hata akija kupata wa
kwake itakuwa ni hivyohivyo.
Heshima kwa kila mtu
Msichana
ambaye anaheshimu kila mtu, mdogo na mkubwa, anawapenda na kuwaheshimu
ndugu, jamaa na marafiki zako, huyu ana sifa ya kuwa mkeo pia.
Anajishusha
Ogopa
sana mwanamke ambaye anataka usawa. Anayekufaa ni yule anayejua yeye ni
mke, na wewe ni mume. Anayetambua kuwa, mwanaume ndiye kiongozi wa
familia.
Anakuongoza kwenye mema
Kama
mpenzi wako ni wa kukutaka kila siku muende baa au mfanye madili hatari
ili mpate pesa, huyu hana sifa ya kuwa mkeo. Mke ni yule ambaye
atakuongoza kwenye kutenda mema na kuacha mabaya.
Kwa
mfano kama unakunywa pombe atakushauri uache, kama siyo mtu wa ibada,
atakushawishi umjue Mungu wako na mambo mengine kama hayo.
Anajua maisha na mapenzi
Mapenzi
yanachukua sehemu kubwa ya maisha ya binadamu. Kwa maana hiyo mwanamke
anayekufaa wewe ni yule ambaye anayajua mapenzi vilivyo lakini pia
anajua maisha.
Kama
yeye ni mtaalam wa majamboz tu lakini linapokuja suala la mambo ya
kimaendeleo hayumo, huyo hafai. Pia akiwa yeye ni mtu wa mambo ya
kimaendeleo tu lakini linapokuja suala la mapenzi ni sifuri, pia
hakufai.