- Home
-
- KUMBE ASILIMIA 75 YA WANAWAKE/WASICHANA WANAKIRI SIMU ZINAVUNJA MAHUSIANO YAO..
KUMBE ASILIMIA 75 YA WANAWAKE/WASICHANA WANAKIRI SIMU ZINAVUNJA MAHUSIANO YAO..

Kama simu yako ya mkononi haikatiki
kiganjani mwako muda wowote, inaweza ikawa inaharibu uhusiano wako na
umpendaye. Wanasaikolojia wamesema kuwa watu wengi kwa sasa wanalazimika
kushindana na smartphone za wapenzi wao kupata attention.
Utafiti uliofanywa, umebaini kuwa robo tatu ya wanawake wanaona kuwa
smartphones zinaingilia maisha yao ya mapenzi na kupunguza muda ambao
wangetumia kuzungumza au kuwa karibu na wapenzi wao. Wanasayansi wamedai
kile walichokiita ‘technoference’ kina madhara makubwa kama migogoro
mingi, kupunguza quality ya uhusiano, kupunguza mridhisho wa maisha na
hatari kubwa ya msongo wa mawazo.
Utafiti huo ulifanywa na mwanafunzi wa chuo kikuu cha jimbo la
Pennsylvania, Marekani na mwingine wa chuo kikuu Brigman Young
University cha Utah na kuhusisha wanawake 143.
Asilimia 62 walisema teknolojia imeingilia muda waliotumia pamoja na
wapenzi wao na theluthi moja wakisema boyfriend zao waliangalia
smartphone wakati wakizungumza.
Wanasayansi hao wameshauri kuweka simu silent na kutokuwa nazo muda wote
ili kuwa na muda wa kufocus kwa mpenzi wako. “Kama unataka kuangalia
kitu muhimu, toa maelezo kwanza na kisha angalia simu yako.
Na pia usijitetee pale mpenzi wako akionesha kukerwa na tabia yako ya
kuangalia sms au kucheza games mara kwa mara – ni njia ya yeye kusema
kuwa angetaka kuconnect na wewe moja kwa moja.
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News