Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi Afunguka Sababu za Kufungwa na Azam

Admin Updates7 months ago5 Views

 

Makocha wa timu za Yanga na Azam FC walitoa maoni yao baada ya Azam FC kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi Kuu.
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, alikiri kushindwa lakini akaeleza kuwa kadi nyekundu iliyotolewa kwa mchezaji wake ndiyo iliyowagharimu zaidi.
“Hakuna anayependa kupoteza lakini inabidi tukubali, hii ni sehemu ya soka,” Gamondi alisema,
Aliongeza kuwa, licha ya kucheza pungufu katika kipindi cha pili, timu yake ilionyesha mchezo mzuri zaidi ya Azam, jambo linalowapa matumaini kwa michezo ijayo.
Kwa upande wake, kocha wa Azam FC, Rachid Taousi, alionyesha furaha kubwa kwa ushindi huo, akisema timu yake imekuwa ya kwanza kufunga goli dhidi ya Yanga msimu huu. Alitambua mchango wa kila mmoja aliyehusika katika ushindi huo muhimu.
“Nautoa ushindi huu kama zawadi kwa mashabiki na bosi wetu,” alisema Taousi.
Katika mchezo huo uliokuwa wa ushindani mkubwa, kiungo wa Azam FC, Adolf Mutasingwa, alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi na alikabidhiwa tuzo yake kutoka Benki ya NBC.
Mashabiki wa Azam walisherehekea ushindi huu ambao umewapa alama muhimu kwenye msimamo wa ligi, huku Yanga wakijipanga kurekebisha makosa kwa ajili ya mechi zijazo. Mechi ilimalizika kwa matokeo ya Yanga 0-1 Azam.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.