KIMENUKA: Kamwe Amchana Ahmed Ally ‘Zungumzia Mechi yako na Al Ahly Achana na Sisi’

Admin Updates1 year ago5 Views

 KIMENUKA: Kamwe Amchana Ahmed Ally 'Zungumzia Mechi yako na Al Ahly Achana na Sisi'

Kamwe amchana Ahmed Ofisa habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amemtaka Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kuzungumzia timu yake na kuacha kuizungumzia Yanga kuelekea michezo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa weekend ijayo katika Dimba la Mkapa.
Kamwe amesema hayo baada ya Ahmed kuiponda Yanga kwa kuweka kiingilio bure kwenye mchezo wao dhidi ya Mameldi Sundowns ambapo amemtaka azungumzie mechi yao dhidi ya Al Ahly na si Yanga kama ambavyo amekuwa akifanya.
“Kila mtu azungumzie mechi yake jamani, sisi hatutaki kumpeleka mtu mjini, kila mtu abaki na mechi yake. Sasa hivi kila wakizungumza kidogo wanaitaja Yanga, tajeni Al Ahly mnaecheza nae, kama sisi tunavyoimtaja Masandawana, tajeni mtu wenu kwa nini mnatufuata fuata sisi? Nyie mnacheza na Al Ahly sio Yanga.
“Sisi Yanga tangu tumeanza hamasa tunamtaja Mamelodi tu, mmeshanisikia mimi nazungumza kuhusu Simba? Nazungumza Mamelodi kwa sababu ndiyo timu tunayocheza nayo. Lakini mtu anaona mechi yake imebuna anawaza aibukie wapi, anaanza kuitaja Yanga, mmeshachelewa.
“Mimi sitaki kumpeleka mtu mjini na sitaki mtu anipeleke mjini, kila mtu azungumzie mechi yake tuone. Tafuta njia yako. Sisi sasa hivi kila mtu simu zinaita, tunaongea na Wasauzi tunawaita hapa kwa Mkapa, na wewe wapigie Waarabu kama una ubavu huo, ongea nao, waite usituingize sisi.
“Serikali imesema tupambane na maaduni jamani, tusipigane wenyewe, wewe si uongee na Mwarabu mnashindwa nini? Mbona sisi tunajiamini tunaongea na Masandawana kwa kujiamini kwamba anakufa kwa Mkapa.
“Lakini mtu anajitokeza anasema wameweka viingilio bure, inkuhusu nini? Kwani mnacheza na sisi? Sisi tunaweza kuweka viingilio bure hata kwenye dabi tukiamua kwa sababu tunaamua wenyewe. Na wewe zungumzia jambo lako usituguse guse sisi, sisi tuna-focus kuifurahisha nchi, mambo makubwa tunataka kuyafanya Jumamosi, mtuache tupumzike tuna kazi kubwa,” amesema Kamwe.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.