KAULI YA WEMA SEPETU YA HIVI KARIBUNI KUWA HAWEZI KUZAA, KAJALA AWAONGOZA MASTAA KUMTULIZA WEMA

Admin Updates10 years ago6 Views



KUFUATIA kauli ya Wema Sepetu ya hivi karibuni kuwa hawezi kupata mtoto
wa kumzaa, mastaa wa fani mbalimbali wamejitokeza kumtuliza moyo,
wakiongozwa na hasimu wake wa karibu, Kajala Masanja, ambaye amesema
hana sababu ya kukata tamaa, kwani bado ni mdogo.


Akizungumza na gazeti hili baada ya kuombwa maoni yake, Kajala alielezea
masikitiko yake juu ya hali ya rafiki yake wa zamani, lakini akasema
anaamini hana tatizo kubwa la kumfanya asipate kabisa mtoto, isipokuwa
anadhani bado hayampata mtaalamu sahihi wa masuala ya wanawake anayeweza
kumsaidia tatizo alilonalo.


“Namuombea sana kwa Mungu, lakini sitaki kabisa kuamini kama hawezi
kupata mtoto katika maisha yake, mbona bado kijana sana, atapata tu
bwana,” alisema Kajala, ambaye ana mtoto aitwaye Paula.“Sitaki kuamini,
 roho inaniuma sana, namshauri Wema asiumie wala kuwa mnyonge. Na watu
waache kumuumiza kwa maneno ya kebehi, lakini kama Wema akiwa tayari
kulea mtoto wa mwenzake, anione, nina imani atapata mtoto atamlea na
kumtunza kama wake.


“Naomba achukue mfano wangu mimi Wastara, Mungu kanipokonya mguu kanipa
watoto, natumia mguu wa bandia na ninatembea lakini Wema amepewa kila
kitu kasoro mtoto, atumie mtoto ambaye siyo wa kumzaa amlee kama wa
kwake na hapo machungu, huzuni na mawazo vitaisha na atamzoa kama wa
kwake,” alisema Wastara Juma.


Wengine waliompa pole na kumtakia nguvu kukabiliana na tatizo lake ni
pamoja na Jini Kabula, Salome Urassa ‘Thea’, Aisha Bui, Amanda Posh na
Baby Madaha ambaye alisema;


“Mtoto siyo mwisho wa maisha, kuna mastaa wengi tu ambao hawana watoto
na wanaishi kwa amani kama Oprah, Tyra Banks na wengineo, hivyo siyo
ishu kubwa kihivyo, watu waache kumsakama Wema, mimi mwenyewe sina
mpango wa kuwa na mtoto.”


-GPL

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.