KALI YA MWAKA HII:MUONE HUYU BIBI WA MIAKA 54 ANAVYOLIA BAADA KUTOROKWA NA MCHUMBA WAKE MIAKA 25

Admin Updates10 years ago5 Views


HARUNI SANCHAWA NA MAKONGORO OGING, PWANI

LILE sakatala lililotamba kwenye vyombo vya habari la  bi harusi, Bahati
Mwakambonja (54), kutaka kufunga ndoa na kijana wa miaka 24, Isiaka
Jeremiah limechukua sura mpya baada ya bwana harusi huyo kutoweka
nyumbani Mkuranga, Pwani na kwenda kusikojulikana huku bibi huyo
akishinda analia.
Bibi Bahati Mwakambonja anayedai kutorokwa na mchumbaake.

Timu ya Amani hivi karibubni ilifika nyumbani kwa mwanamke huyo mjini
Mkuranga na kumkuta katika lindi la mawazo.Akizungumza na gazeti hili
kwa masikitiko makubwa, Bahati alisema: “Mchumba wangu kakimbia jamani.
Niliwashangaa sana viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) Kurasini (Dar) kukwamisha ndoa yangu na yule mchumba wangu,
nimehuzunika kwa kiasi kubwa hadi sasa.

“Kwanza nikiri kwamba mimi sizai, hiyo ni mipango ya Mungu, huwezi
kulazimisha hali niliyonayo. Tumekaa kwa muda mrefu bila kufunga ndoa
lakini ilifikia hatua tukaamua kitu ambacho hata kwa Mungu ni baraka
kwetu lakini matokeo yake imekuwa  kinyume,” alisema mwanamke huyo.

Bibi huyo alisema kama kuolewa na huyo kijana alishaolewa kwa sababau
walishaenda sehemu zote  mbili, yaani nyumbani kwa mwanaume na kwa
mwanamke.“Mume wangu alifanya mazungumzo na familia yangu na kuhojiwa
maswali kadhaa ambayo aliyajibu na kuambiwa atoe mahari kitu ambacho
alifanya kwa kutoa sehemu ya mahari.

“Hatua tuliyokuwa tunakwenda ndugu waandishi ya kukamilisha taratibu za
ki-Mungu ambapo tunajua kila mtu ana sehemu anayoiabudu  hapa duniani na
mimi nilikwenda pale kwa sababu ni eneo ambalo nilikuwa nikipata 
huduma kabla ya kuhamia hapa Mkuranga.

“Lakini baada ya kufika eneo lile nikaambiwa mambo ambayo nilikuwa
siyategemei hata siku mmoja, likiwemo la kuwasilisha barua ya talaka au
cheti cha kifo cha mume wa kwanza.“Mimi niliachana na mume wa kwanza kwa
muda  mrefu sana na alinikataa kwa sababu sizai na kuwaambia wale
waliosimamia ndoa ya awali kuwa anawaruhusu kama nikipata mchumba
niolewe,” alisema Bahati.

Aidha, alisema kuna watu waliwafuata wakiwaahidi watawasaidia ili
kufanikisha kufungwa kwa ndoa hiyo lakini matokeo yake baada ya wao
kuondoka walishitukia taarifa hizo ziko kwenye magazeti.
Alisema baada ya Isiaka kuona taarifa hizo kwenye gazeti alitoweka na baadhi ya vielelezo kama picha walizopiga siku za nyuma.

“Mimi kama mtu mzima nimechaganyikiwa hasa baada ya ndoa yangu
kukataliwa sehemu zote nilizokwenda na kibaya zaidi ni pale mume  wangu
kuondoka na vitu muhimu kwenda nisikokujua, hana simu.Uchunguzi wa
gazeti hili ulibaini kuwa, mama huyo kwa sasa anajitafutia kipato cha
kila siku kwa kufundisha watoto wadogo wapatao 8 ambao kila baada ya
kufundisha hulipwa shilingi 200 kwa siku. Alisema kuwa hana uchumi
mwingine.

Alisema uhusiano wake na kijana huyo ulianza baada ya kukaa kwa muda
mrefu bila kuolewa lakini chanzo kikubwa kilichomkutanisha na Isiaka ni
ugonjwa wa kisukari uliyokuwa unamsumbua kwa muda mrefu.
Alisema yeye
na mume wake wa kwanza walioana mwaka 1992 na kuachana 1995. Alikaa
hapo mpaka Januari 2003 alipokutana na kijana huyo.

Aliongeza kuwa walipokutana na kijana huyo hawakuanza uhusiano moja kwa
moja lakini baada ya kuona  anampa msaada ambao hata mbele za Mungu
inakubalika ndipo waliamua kuingia katika uhusiano wa kimapenzi hatimaye
kulipa mahari na hatimaye kanisani ambako walikataliwa kutokana na
tofauti ya umri.

Baadhi ya majirani waliozungumza na Amani kuhusiana na sakata hilo walisema:
 “Ni kweli kijana huyo alikuwa akionekana  eneo hilo na kila mtu alijua ni mfanyakazi wa mama huyo.
“Hakuna aliyefikiria kijana huyo ndiye mume wa mama huyo,” alisema jirani mmoja.

Amani lilimtafuta Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Ushirika wa Kurasini, Dar, Yusuf Ngelein ambapo alikiri
kumfahamu Bahati kama muumini wake.“Alifika hapa na mwenzake kutaka
taratibu za kufunga ndoa. Mimi kama kiongozi wa kanisa nilimpa vigezo
vya kutimiza lakini hawakurudi maana yake walikuwa na upungufu,” alisema
mchungaji huyo
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.