Jinsi ya kupata kitu unachokitaka na kwa wakati muafaka

Admin Updates8 years ago7 Views

Jinsi ya kupata kitu unachokitaka kwa wakati muafaka

Wengi wetu huwa tuna fikra na imani potofu zinazokwamisha
mafanikio ya malengo yetu binafsi. Huwa kama vizuizi vya njia ya mafanikio kati
yetu na maisha tunayoyataka. Nina imani kila mmoja wetu ana hulka ya kumiliki
kitu au vitu anavyovitaka. Ni rahisi sana kutafakari na kutamani vitu
unavyovitaka kuliko kuvifanikisha.


Kama ingekuwa rahisi kupata vitu unavyovitaka, nadhani kusingalikuwa na haja ya
kuhitaji chochote – Si Ndio? Ukweli ni kwamba hakuna njia iliyonyooka ya
kuvipata unavyovitaka bali leo nitakushirikisha baadhi ya mbinu muhimu
zitakazokusaidia kurahisiha ufanikishaji wa kupata kitu au vitu
unavyovitaka katika namna moja au nyingine.

Hii inaweza kuonekana kama jambo la kawaida sana, lakini
mengi wetu wana tatizo la kushindwa kuomba kitu wanachokitaka. Je, unataka
kulipa kuongezewa malipo? Je, unataka kujua kama mpenzi uliyempata
anakupenda kwa dhati? Jiamini, nenda kwa muhusika, na kisha umuulize. Hii
inaweza kuwa njia rahisi kabisi ya kupata unachokitaka.

Watu wengi huchelewa kupata vitu wanavyovitaka kwasababu ya
kupoteza muda mwingi katika kusubiria 
“wakati
muafaka.” 
Naam, kama utakuwa mtu wa kusubiri wakati
muafaka, kuna wakati mwingine utalazimika kupoteza muda mwingi katika subira
yako. Wakati mwingine unapaswa kukifuata tu kitu na kukipata.
Isipokuwa kama una sababu nzuri na ya kweli ya kusubiri.

Moja ya njia mahususi ya kufanikisha kupata kitu unachokitaka ni
kufanya mpango madhubuti tena kwa kuuandika katika kitabu chako cha kumbukumbu.
Orodhesha malengo yako kisha uyaandike chini. Kuandika lengo lako katika
karatasi ndio dhamira kuu hapa. Na kwa kila lengo ulilonalo, jiwekee mpango wa
utekelezaji wenye utaratibu unaoeleweka wa kutekeleza malengo yako, pia
hakikisha unalifanyia kazi lengo lako kila inapoitwa leo.

Zingatia kupata unachokitaka. Epuka vikwazo visivyo vya lazima,
zingatia muda na pia zielekezee nguvu zako katika utekelezaji wa kupata
unachokitaka. Na usijilinganishe na watu wengine – Hiyo ni sawa na kujifungulia
akaunti ya matatizo.Weka mkazo juu yako mwenyewe na juu ya kile unachoweza
kukifanya kutekeleza malengo yako.

Jua unachokitaka, kwa marefu na mapana. Jenga picha akilini mwako
kuwa umekipata unachokitaka na kisha jiaminishe kuhusu jambo hilo. Ishi ukiwa
na fikra chanya kuwa utapata unachokitafuta. Bila shaka, huwezi kuishia kuamini
tu bali utatakiwa ufanye kazi kwa bidii, maarifa na uaminifu mkubwa ili
ufanikishe malengo yako.

Tenga muda fulani kila siku kujenga taswira ya maisha baada ya
mafanikio ya kile unachokitafuta. Jenga akilini mwako kuwa umekipata kile
ulichokuwa unakitafuta. Kwa kufikiria na kukumbuka mafanikio ya lengo lako
inakupa urahisi wa wewe kulifikia lengo lako. Vilevile kwa kujijengea taswira ya
mafanikio akilini mwako, inakufanya ujiamini na kuamini kuwa unaweza kuyafikia
malengo yako.

Jenga uhusiano na watu madhubuti. Jumuika na watu ambao tayari
wapo kwenye nafasi unayoitaka, au wamepata mafanikio ya kitu unachokitaka,
watakuwa msaada wa pekee sana kwako. Ni jambo jema daima kuwa na uhusiano
na urafiki chanya  hasa linapokuja suala la kufikia malengo yako – hasa
katika kazi yako.

Ndiyo, mambo yajayo – daima huwa yanatia hofu. Vipi kama
usipofanikiwa kupata kitu unachokitaka? Vipi kama ukishindwa? Na maswali
mengine mengi kama hayo. Cha msingi ni kutoruhusu hofu yoyote ikuzuie
kutekeleza mipango yako. Lakini, vipi kama ukifanikiwa kupata kile unachotaka?
Vipi kama ukikipata? Ukweli ni kwamba mis siyajui mawazo yako juu yamafanikio
yako mwenyewe, lakini kwa upande wangu mimi nachagua kuishi na maswali ya Vipi
kama nikifanikiwa?

Wakati mwingine unatakiwa ukubaliane na matokeo ya kile
unachokipata.  Huwezi kuwa unapata kila kitu katika hali unayoitaka daima.
Kama umefanya kazi kwa bidii, maarifa na uaminifu wako, na bado ukajikuta
haujafanikisha lengo lako, Usikate tamaa! Kubaliana na hali halisi kisha songa
mbele kwa kuweka lengo jipya na kufuata mpango wa utekelezaji.
$ Omba
$ Achana na tabia ya kusubiri “wakati muafaka”
$ Fanya mpango
$ Zingatia
$ Amini –
$ – na Uvutie taswira
$ Jumuika na ujenge uhusiano
$ Chukua hatua sasa
$ Kubaliana na matokeo kisha songa mbele

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.