Jeshi la Polisi Labuni Mkakati Maalumu Kukabili Ajali za Viongozi na Watumishi wa Umma

Special Correspondent6 years ago5 Views

Ili kudhibiti wimbi la ajali za barabarani zikiwamo zinazohusisha gari za viongozi na watumishi wa umma, Jeshi la Polisi jijini Dodoma limeeleza mikakati yake ikiwamo kuwapa mafunzo ya muda mfupi.

Hayo yalielezwa jijini hapa jana na Kamanda wa Polisi Dodoma, Gilles Muroto, ofisini kwake alipozungumza na waandishi wa habari walio katika mradi wa usalama barabarani unaosimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

“Dodoma ni mji mkuu na makao makuu ya nchi, viongozi wengi wa Serikali wamehamia hapa akiwamo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na wakuu mbalimbali wa nchi.

“Shughuli nyingi za kitaifa zinafanyika hapa, kwa msingi huo tunahakikisha tunaimarisha usalama kila kona hadi huko barabarani, wanakuja salama na kuondoka salama, hakuna ajali,” alisema.

Alisema ili kuhakikisha madereva wa viongozi na watumishi wa umma wanaendelea kuendesha kwa usalama wanawapa mafunzo ya miezi mitatu.

“Hivi karibuni kulikuwa na changamoto ya ajali, tumechukua hatua, tunawaita, wanakaa kwenye bwalo letu pale tunawafundisha, lengo ni kuwakumbusha maana mtu anaweza kuwa amepata leseni muda mrefu,” alisema.

from MPEKUZI http://bit.ly/2PWtlcN

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.