Wanakutana mastaa wawili
wa Bongo Movies, kwenye filamu ya KAUVA na kufanya makubwa ni hatari
unajua wasanii hao ni nani nani? Basi si wengine ni Jack Wolper na
kipenzi cha wengi mzee wa Malavudavi Haji Adam aka Baba Haji stringi wa
Kihindi
Filamu ya Kauva inatarajia kuleta mapinduzi katika tasnia ya
filamu kutokana na Teknolojia iliyotumika katika utengenezaji uigizaji
na wasanii walioshiriki katika filamu hiyo kuigiza wameonyesha ushindani
mkubwa sana anasema msemaji wa Splash Steve Serengia.
“Ni kazi ambayo imetengenezwa na kutedewa haki na wasanii walioigiza
kama unavyomjua Baba Haji na amekutana na Jack Wolper huku kuna Hashim
Kambi si mchezo na inasambazwa na Splash Entertainment,”anasema Steve.
FC