Huu hapa Wasifu wa bosi Mpya Wa Idara Ya Usalama Wa Taifa Balozi Ali Idd Siwa

Special Correspondent1 year ago6 Views

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa Balozi Ali Idd Siwa amekuwa katika utumishi wa umma tangu mwaka 1977 na kati ya mwaka 2001-2014 Ndugu Siwa alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi iliyoko Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates); Moscow, nchini Urusi na baadaye Berlin, nchini Ujerumani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2023.

Ndugu Ali Idd Siwa Agosti, 2014 Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kigali, nchini Rwanda akichukua nafasi ya Balozi Dkt Mwita Marwa Matiko. Majukumu aliyoendelea nayo pia mwaka 2018-2021 baada ya kuteuliwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli kabla ya kurejea nchini na kuteuliwa kuiongoza bodi ya Mfuko wa NSSF na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Katika nafasi mbalimbali alizotumikia ametajwa kuwa mtu mahiri katika utendaji kazi wenye uadilifu, uzalendo, ubunifu na matokeo makubwa.

Masama Blog inamtakia kila la Kheri katika majukumu yake ya kusimamia na kulinda maslahi ya Usalama wa taifa letu Balozi Siwa.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.