HII NDIYO STORI A TO Z KUHSU DIAMOND KUMPA MIMBA ZARI!!!

Admin Updates10 years ago5 Views

 
BAADA ya kufunguka kuwa zilipendwa wake, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’,
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Penniel Mwingilwa ‘Penny’ wamegoma kumzalia,
habari ya mjini kutoka kwa mfalme wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ ni kwamba anadaiwa kumdunga mimba mpenzi wake wa sasa, Zarinah
Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’, Ijumaa linakupa ubuyu wa motomoto.

 

Mfalme wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi na mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari’. CHANZO CHAVUJISHA MCHAPO
Wiki
mbili zilizopita, chanzo kilicho karibu na Diamond kiliwalipenyezea
mchapo mapaparazi wetu kuwa uhusiano wa Zari mwenye maskani yake Uganda
na Afrika Kusini ‘Sauzi’ na jamaa huyo tayari umejibu hivyo mashabiki wa
mastaa hao wategemee ujio wa uzao wa wawili hao.

“Hivi habari
ya Zari kuwa mjamzito mnayo? Mbona iko wazi na Diamond amefurahi sana
maana si unajua tena alihangaika sana kupata mtoto kwa Wema, Jokate na
Penny wote wakamzingua? Sasa habari ya mjini ndiyo hiyo,” kilidai chanzo
hicho huku kikiomba chondechonde kistiriwe jina.

DIAMOND ATHIBITISHA KIAINA
Wakati
wanahabari wetu wakiendelea kuchimba undani wa habari hiyo, usiku wa
kuamkia Jumatano iliyopita, Diamond alitupia picha kwenye ukurasa wake
wa Mtandao wa Instagram iliyoashiria kwamba anathibitisha yale
yaliyovujishwa na chanzo chetu kuwa yana ukweli.

PICHA ILIKUWAJE?
Picha
hiyo aliyoitupia Diamond ilikuwa ikimuonesha mtoto wa kike, Zari akiwa
amelala kwenye mapaja ya Diamond ikiwa imeambatanishwa na picha ya
‘Ultrasound’ kuonesha tumbo la Zari lina kiumbe kilichoanza
kurutubishwa.

Picha ya ‘Ultrasound’ ikionesha tumbo la Zari kuwa na kiumbe ndani yake.

 
 ASINDISIKIZA NA UJUMBE
Chini ya picha hiyo, Diamond alisindikiza na na ujumbe ulisomeka hivi:
“I can not wait to have you on my hand…# Chibu_Junior.”
(Siwezi kusubiri kukubeba mikononi mwangu Chibu Mdogo)

AITOA MTANDAONI
Katika
hali ya kushangaza, wakati wapenda ubuyu wachache wakiwa ‘wameshaiiba’
picha hiyo mtandaoni, Diamond aliitoa fasta ikidaiwa kuwa alishauriwa
kufanya hivyo.
“Atakuwa kashauriwa aitoe maana si unajua tena Wabongo
wangeanza kumshambulia, akaona bora atoe fasta,” aliandika mmoja wa
wadau wa Diamond mtandaoni. ZARI NAYE ATUPIA
Kwa mujibu wa mitandao
mbalimbali nchini Uganda, mara baada ya Diamond kuposti picha hiyo, Zari
naye aliichukua na ‘kui-repost’ katika akaunti yake kisha na yeye
kuitoa baada ya muda mfupi.

YAWA GUMZO UGANDA
Baada tu ya
Zari kuposti na kuitoa picha hiyo, vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa
vikijadili picha hiyo na kufanya mastaa hao wawe gumzo nchini humo huku
wadau mbalimbali wakitoa maoni yao.

“Tunampongeza Diamond kwa
kuunganisha undugu kati ya Tanzania na Uganda, kama wamekubaliana wazae
tu hakuna shida,” ilisomeka sehemu ya maoni lukuki mtandaoni juu ya ishu
hiyo.


Shemeji yetu kwa ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ akijiachia. 
 
DIAMOND ANASEMAJE?
Wanahabari wetu walimuibukia kwa zaidi ya mara
tano Diamond nyumbani kwake, Sinza-Mori jijini Dar lakini hakuwepo,
baadaye alipatikana kwenye simu na kujibu kwa kifupi:
“We kama umeona kwenye akaunti yangu unauliza nini tena?”

MTU WA KARIBU
Ili
kuzidi kuchimba ukweli wa habari hiyo, wanahabari wetu walimvutia waya
mtu wa karibu wa Diamond ambaye hakupenda kuanika jina gazetini lakini
akakiri kuwa Zari ana mimba ya Diamond.

“Mbona kitambo tu,
Diamond alivumilia kwa muda mrefu lakini jana usiku (Jumanne kuamkia
Jumatano) ndiyo akaamua kuweka picha kisha akaitoa,” alidai mtu huyo wa
karibu na Diamond.

KUMBUKUMBU
Kabla ya habari hiyo ya mimba
ya Zari, huko nyuma Diamond aliwahi kuambiwa hana uwezo wa kumpa mimba
mwanamke lakini mwenyewe alifafanua kwamba wachumba wake wote
‘aliobanjuka’ nao kwa nyakati tofauti, waligoma kumzalia kwa kile
alichokiita ni kupenda ‘utoto wa mjini.’

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.