HII NDIYO KAULI YAMAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU KUHUSU WATUMISHI WA AFYA WANAOIBA DAWA ZA SERIKALI.

Admin Updates9 years ago5 Views

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan amewaonya baadhi ya watumishi wa sekta ya afya nchini kujiepusha na tabia ya kuuza dawa zinazopelekwa na serikali kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali kwani hali hiyo inaweza kusababisha manung’uniko kwa wagonjwa na wananchi kuichukia serikali yao.
 
Alitoa onyo hilo jana alipotembelea na kuzindua majengo ya hospitali teule ya Rufaa ya mkoa wa Geita, yaliyokarabatiwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) kwa gharama ya jumla ya shilingi milioni 271, ambapo mgodi wa GGM umechangia shilingi milioni 212 na serikali imetoa shilingi milioni 59.

Kwa upande wake waziri wa afya, maendeeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu alikiri kuwepo kwa wizi pamoja na upotevu wa dawa za serikali kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji na uadilifu miongoni mwa watumishi wa sekta ya afya.

Hospitali hiyo teule ya Rufaa ya mkoa wa Geita inatarajiwa kuhudumia zaidi ya watu 1,700,000 wanaoishi katika mkoa huo kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, kabla ya kuwa hospitali ya rufaa ilikuwa ikihudumia zaidi ya watu laki nane wa halmashauri ya Geita.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.